25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 1, 2024

Contact us: [email protected]

CASSPER NYOVEST AMTUMIA VANESSA KUPENYA AFRIKA MASHARIKI

NA MWANDISHI WETU

STAA wa singo ya Doc Shebeleza kutoka Afrika Kusini, Refiloe Phoolo (Cassper Nyovest) amemtumia msanii Vanessa Mdee kama ‘Video Queen’ katika video yake mpya ya Baby Girl, aliyoitoa juzi lengo likiwa ni kupata mashabiki wapya kutoka ukanda wa Afrika Mashariki.

Mwaka huu rapa huyo ameonekana kulitamani soko la muziki la Afrika Mashariki ambapo amekuwa akifanya kazi na wasanii kama Diamond Platnumz katika msimu uliopita wa Coke Studio na Julai mwaka huu alipokewa kwa shangwe na mashabiki wa Bongo Fleva katika tamasha kubwa la Castle Unlock lililofanyika nchini mwezi Julai.

“Video ya Baby Girl Music tayari imetoka na ndani yupo msichana mzuri na mwezi kipaji Vanessa Mdee,” Cassper Nyovest alimsifia Vanessa kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Naye Vanessa Mdee amesema kuwa video hiyo ya Baby Girl ni mwanzo wa kazi endelevu zitakazokuja kati yake na rapa Cassper Nyovest.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles