Mume aiba figo ya mkewe kujilipia mahari India

0
1239

TAMADUNI nyingi nchini India mwanamke ndiye anayewajibika kulipa mahari ili kuolewa tofauti na maeneo mengine duniani, ambayo hufahamika suala hilo liko mikononi mwa mume.

Hata hivyo, malipo ya mahari hiyo ambayo hulipwa familia ya mume kutoka kwa familia ya mke nchini India yamepigwa marufuku nchini India tangu mwaka 1961.

Pamoja na marufuku hiyo, vitendo hivyo bado vinaendelezwa katika jamii nyingi kiasi cha kugeuka kama biashara.

Kwa mfano, wanawake wenye sura mbaya au ulemavu hutakiwa kulipa mahari kubwa kwa familia ya kiume ili waweze kuolewa.

Katika kisa kilicho kusudio la makala haya, mume na nduguye wa kambo wamekamatwa baada ya kushukiwa kumuibia figo mwanamke wa mume huyo ili kujilipia mahari, ambayo awali haikuwa imelipwa.

Vyombo vya habari vimeripoti kwamba mumewe mwanamke huyo kutoka Magharibi mwa Bengal alipanga upasuaji wa eneo moja la tumbo lake wakati alipokuwa akiugua uchungu.

Baadaye mwaka 2017, alifanyiwa vipimo viwili, ambavyo vilibani kwamba figo yake moja haipo.

Amemshuku mumewe kwa vile mara kwa mara alitaka kulipwa mahari yake, hatua ambazo ziliambatana na mateso.

Akizungumza na vyombo vya habari nchini India, mwathirika wa tukio hilo, Rita Sarkar, alisema amekuwa katika mgogoro wa kinyumba kutokana na mahari hiyo kwa miaka mingi.

”Mume wangu alinipeleka katika hospitali binfasi mjini Kolkata, ambapo yeye na maafisa wa afya waliniambia kwamba atapona atakapotolewa eneo hilo la kidole tumbo lililovimba kupitia upasuaji,” gazeti la Hindustan lilimnukuu akisema.

Anasema kuwa mumewe alimuonya kutozungumza kuhusu upasuaji huo kwa mtu yeyote mjini Kolkata.

Miezi kadhaa baadaye mwanamke huyo alikuwa akihisi vibaya na akapelekwa hospitalini na watu wa familia yake.

Uchunguzi ulibaini kwamba figo yake ya upande wa kulia ilikuwa imetolewa na uchunguzi wa pili ulithibitisha ukweli huo.

”Baadaye nikabaini sababu ya mume wangu kunitaka nisizungumzie upasuaji niliofanyiwa’, aliambia gazeti la Hindustan Times.

”Aliuza figo yangu kwa sababu familia yangu haikuweza kumlipa mahari yake”.Mwanamke huyo alisema na sasa mumewe na nduguye wa kambo wamekamatwa kwa kitendo hicho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here