Mtoto wa Kylie aonyeshwa kwa mara ya kwanza KUWTK

0
776

LOS ANGELES, MAREKANI

MTOTO wa mwanamitindo wa Marekani, Kylie Jenner, Stormi, ameonekana kwa mara ya kwanza katika tamthiliya inayohusu maisha ya familia ya Kardashian.

Uamuzi huo unakuja baada ya kuwapo kwa siri tangu Kylie awe na ujauzito wa mtoto huyo ambaye alijifungua Mei mwaka huu.

Lakini Jumapili iliyopita, mwanamitindo huyo alimuonyesha hadharani wakati akimkaribisha Stormi katika familia hiyo ambayo imeamua kuweka wazi maisha yao kupitia kipindi cha ‘Keep Up with  Kardashians (KUWTK).’

“Sikuwa nimeweka siri kuhusu ujauzito wangu ila nilifanya  vile kwa manufaa yangu binafsi,” Kylie alimweleza mpigapicha wa  KUWTK.

Akizungumzia kitendo hicho, dada wa mwanamitindo huyo, Kim alisema: “Kylie alitaka kuwa mama, hivyo  kumpata mtoto Stormi ni jambo la furaha kwake, binafsi nimependezwa na kitendo cha kupata motto, nina uhakika atakuwa mama bora.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here