24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Moto wateketeza hoteli ya mtoto wa Amani Karume

Na Khelef Nassor, Zanzibar

MOTO  umeteketeza hoteli ya Kitalii ya Konokono Beach Resort iliyopo Kijiji cha Michamvi Mkoa wa Kusini Unguja na kusababisha hasara ya zaidi ya Sh milioni 400.

Hoteli hiyo inayomilikiwa na mtoto wa Rais mstaafu wa awamu ya sita wa Zanzibar, Amina Karume, iliteketea jana kwa moto huo ambao chanzo chake ni vijana wawili waliokuwa wakichoma majani jirani   na hoteli hiyo.

Akizungumza na MTANZANIA kuhusu moto huo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Juma Saadi, alisema moto huo umeteketeza hoteli hiyo inayomilikiwa na   wawekezaji watatu akiwamo mwekezaji mzalendo, Amina Karume na Wataliani wawili, ambao ni Andrea Schampo na Luca Gambirula.

Alisema moto huo umeteketeza nyumba tatu   na mgahawa mmoja   ndani ya hoteli hiyo.

Kamanda Saadi, alisema baada ya kupata taarifa za moto huo, jeshi la polisi kwa kushirkiana na kitengo cha Zimamoto, waliwahi katika eneo la tukio na kuuzima.

Alisema chanzo cha moto huo ni watu wawili  waliokuwa wakichoma majani ambao ni Meshak Amos Elisha (50) na Mohammed Abdalla Hassan.

Alisema watu hao walikuwa wakichoma majani hayo katika eneo la hoteli hiyo na Zamzam Maalim Rashid, mkazi wa  Dar es Salaam.

“Wakati wa kuchoma moto ndani ya uzio huo, ulizuka upepo mkali majira ya saa tano na nusu na ukasababisha moto ule kuruka juu na kusababisha  nyumba moja ya makuti   karibu na hoteli ile kuungua moto na kusababisha hasara hiyo,”  alisema Kamanda Saadi.

Hata hivyo, aliwataka wananchi kupuuza taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa kwa kulihusisha tukio hilo na masuala ya siasa.

Vipeperushi vyazagaa

Katika hali ya kushangaza jana mjini wa Unguja,  vipeperushi  vilionekana katika maeneo mbalimbali ambayo kuna wafuasi wa CUF.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles