23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mgonjwa apasuliwa busha lenye kilo 30

 VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

MKUU wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva, amesema ameshangazwa alipoelezwa yupo mtu mmoja amefanyiwa upasuaji wa kuondoa busha lililofikia uzito wa kilo 30.

Kauli hiyo aliitoa jana alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dares Salaam, Paul Makonda kuzindua kampeni ya kitaifa ya unywaji dawa kinga dhidiya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, ikiwamo matende na mabusha ama ngirimaji.

 “Hii yote ni kwasababu ya uelewa mdogo wa jamii juu ya magonjwa haya hali inayochangia wale wanaougua kutokuwahi matibabu mapema, wakiona ni ufahari, wanaona ni umwinyijambo ambalo si kweli,” alisema.

Alisema magonjwa hayo yanasababisha ulemavu na hatimaye kifo.

 “Matende na mabusha, usubi, kichocho, trakoma yamo katika kundi la magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, yote haya husababisha ulemavu na kifo.

“Yalileta mahangaiko, yalipunguza uwezo wa wananchi kushiriki shughuli za kitaifa, watoto wengi walishindwa kuhudhuria masomo, kimsingi afya ni mtaji, kama inazorota mtu hawezi kufanya shughuli zake,” alisema.

Alisema kwa msingi huo Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imejizatiti kuhakikisha wananchi wanapata kinga na tiba.

 “Lengo ni kutumia rasilimali chache ilizonazo kuyadhibiti magonjwa hayo, naipongeza wizara, imelenga kufikia wananchi milioni tano awamu hii ya kampeni, Temeke tumekusudiakuwafikia watu milioni 1.2.

“Nawasihi wananchi wajitokeze kwa wingi, dawa kinga hizipia zinasaidia kukabili upungufu wa damu, zinaepusha upofu, zinapunguza uwezekano wa jamii kupata maambukizi, kuepusha magonjwa ya ngozi na huua vilevimelea vya magonjwa haya ndani ya mwili, na hupata virutubisho muhimu,”alisema.

Awali Mratibu wa Taifa wa Mpango wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele, Dk. Upendo Mwingira, alisema kwa Dar es Salaam jumla ya vituo 923 vitatoa huduma hiyo.

 “Kati yake vituo vyaafya ni 671 na 152 vya kuhamahama, watoa huduma watapita katika maeneo ya mikusanyiko, sokoni, vituo vya mabasi na kwengineko,” alisema.

Aliwatoa hofu Watanzania kwamba dawa hizi ni salama na unywaji wake na wale watakaohitaji upasuaji watafanyiwa bila malipo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles