Imechapishwa: Fri, Jun 8th, 2018

MFUMUKO WA BEI WAFIKIA ASILIMIA TATU

Veronica Romwald, Dar es Salaam

Mfumuko wa bei mwezi uliopita, umepungua hadi kufikia asilimia 3.6 ikilinganishwa na asilimia 3.8 ilivyokuwa mwezi Aprili mwaka huu.

Imeelezwa kupungua huko kwa kiasi kikubwa kumechangiwa na kupungua kwa mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula kama mahindi, unga wa mahindi, mtama, mihogo, unga wa mihogo na viazi mviringo.

Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraim Kwesigabo amesema hayo leo Ijumaa Mei 8, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya mfumuko wa bei wa mwezi.

“Mahindi yamechangia kwa asilimia 10.3, unga wa mahindi kwa asilimia 12.5, mtama kwa asilimia 13.8, unga wa muhogo kwa asilimia 15.2, viazi mviringo kwa asilimia 9.0 na mihogo mibichi kwa asilimia 12.6,” amesema.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

MFUMUKO WA BEI WAFIKIA ASILIMIA TATU