23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

MEYA AKAMATWA AKIPINGA MUSEVENI KUTAWALA MAISHA

KAMPALA, UGANDA

MEYA wa mji mkuu wa Uganda, Kampala, Erias Lukwago, amekamatwa jana asubuhi baada ya kuongoza maandamano ya kupinga kuondoa ukomo wa umri wa anayepaswa kugombea urais.

Wabunge wa Chama tawala cha National Resistance Movement (MRM), wako katika kampeni za kuondoa ukomo wa kuwania urais ili kumwezesha Rais Museveni aweze kuendelea kugombea.

Katiba ya sasa inakataza mtu anayevuka miaka 75 kuwania urais, huku Museveni aliye madarakani tangu 1986 akiwa ameshafikisha miaka 73.

Kwa maana kwamba iwapo ukomo huo hautaondolewa, Museveni hataweza kugombea katika uchaguzi ujao.

Polisi inasema wamebaini fulana zilizochapishwa maneno ya kupinga kikomo cha umri wa rais katika ofisi zake za City Hall.

Juhudi za vyombo vya habari kumtafuta meya huyo ili kuzungumzia tuhuma hizo, zilishindikana kwa vile yuko mahabusu.

Kukamatwa kwa Meya Lukwago, ambaye aligombea udiwani hatimaye umeya kama mgombea binafsi, kunakuja wakati Mbunge Raphael Magyezi wa NRM akitarajia kuwasilisha hoja yake bungeni, akitaka apewe kipindi cha mapumziko kuandaa muswada wa kuondoa kikomo cha umri wa rais.

Kuna hali ya wasiwasi kote Kampala, huku polisi wakiwa wamesambazwa jijini humo.

Polisi wa kikosi cha kupambana na ugaidi wamezingira jengo la Bunge huku askari polisi wengine wakifanya doria.

Mwandishi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) aliyeko hapa, Patience Atuhaire, alisema hata wabunge wanaoingia bungeni wanapekuliwa na maofisa wa usalama kabla ya kuingia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles