25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

May auangukia Umoja wa Ulaya

LONDON, UINGEREZA

WAZIRI Mkuu wa Uingereza Theresa may amewasihi viongozi wa Umoja wa Ulaya (EU) wanaokutana mjini Salzburg kutoweka masharti magumu kwa taifa lake.

Wakati wa chakula cha usiku juzi, May aliwaambia  viongozi wenzake wa EU kuwa kilicho muhimu kwa sasa ni umoja huo kutafuta msingi wa pamoja wa maridhiano kuhusu kujitoa kwa Uingereza ifikapo Machi 29 mwaka ujao.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanajaribu kuamua  ni kwa umbali gani wafikie maridhiano na May ili aweze kuwa na sauti kubwa nyumbani juu ya suala hilo.

Hiyo pia inatokana na upinzani anaokabiliwa nao hasa na wabunge wa chama chake cha Conservative wanaopinga ushirikiano wa karibu na EU wakati taifa hilo litakapoondoka rasmi kutoka umoja huo.

May hakuwepo jana katika majadiliano hayo yaliyohudhuriwa na viongozi wa Umoja wa Ulaya kuhusu suala hilo.

Wakati wa chakula hicho cha siku, May aliwatolea wito viongozi wa Ulaya kuachana na kile alichokiita ‘masharti yasiyokubalika’ ya Brexit, ambayo amesema yanaweza kuisambaratisha Uingereza.

May aliuomba umoja huo kuushughulikia kwa ukarimu mpango wake mahsusi na unaoweza kufanikiwa.

“Na kama tutafikia hitimisho la mafanikio basi kama tu Uingereza ilivyoubadili msimamo wake, EU utahitaji kuubadili msimamo wake pia. Lakini nina matumaini kuwa tukiwa na nia nzuri na ujasiri tunaweza kuafikiana kuhusu mkataba ambao ni mzuri kwa pande zote,” alisema.

Masuala muhimu yanayojadiliwa na wajumbe ni pamoja na mpaka wa Ireland.

Bila kufikia makubaliano, sheria za Umoja wa Ulaya hazitatekelezwa nchini Uingereza, na hiyo huenda ikasababisha vurugu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles