24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

MAWAKILI: CHEBUKATI ALIBORONGA KUSIMAMIA UCHAGUZI

NAIROBI, KENYA

MWENYEKITI wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Wafula Chebukati ameshambuliwa na mawakili wanaowakilisha walalamikaji wa kesi ya kupinga wanaopinga uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26, akidaiwa kuboronga kuusimamia.

Chebukati alitajwa kuwa kinyonga, aliyekuwa akibadilikabadilika na kuwafanya wapiga kura na viongozi kutokuwa na imani naye.

Mawakili hao Aulo Sowetto, Eunice Lumalla na Waikwa Wanyoike waliwaeleza majaji sita wa Mahakama ya Juu kuwa taarifa alizotoa Chebukati hadharani kuwa hana uhakika iwapo IEBC ingefanya uchaguzi huru na wa haki, ziliutia doa uchaguzi huo.

Lumalla alimwambia Jaji Mkuu David Maraga na wenzake watano kuwa, taarifa hizo pamoja na barua, ambazo  Chebukati aliwaandikia maafisa wa IEBC zimeonesha wazi alikuwa kigeugeu.

Wakili Lumalla alisema tabia hiyo ya Chebukati iliwatia wengi hofu, hasa alipokiri hadharani kuwa aliyekuwa Kamishna Dk. Roselyn Akombe alikuwa ametishiwa maisha.

Pia Soweti alisema Chebukati alihutubia wanahabari na kusema vifo na vitisho dhidi ya maofisa wa IEBC vilimfanya kutokuwa na imani na makamishna na wafanyakazi wa IEBC.

“Unamaanisha tabia ya Chebukati ya kuwa kigeugeu iliathiri zoezi hili la uchaguzi wa Oktoba 26, 2017?” Jaji Isaac Lenaola alimwuliza Soweto.

Wakili huyo alijibu “Ndio” na kuongeza hiyo ni sababu tosha ya kuharamisha uchaguzi huo.

“Na pia hakuna anayejua idadi kamili iliyopiga kura wakati wa uchaguzi huu wa Oktoba 26, 2017 kwa vile Chebukati alikuwa anatoa idadi tofauti tofauti,” alisema Wanyoike.

Kesi mbili za Harun Mwau, Njonjo Mue na Khelef Khalifa wanaopinga uchaguzi wa Rais Kenyatta, zinasema haukufanywa kwa mujibu wa sheria za uchaguzi na Katiba.

Watatu hao walisema kauli ya Chebukati kutokuwa na imani na IEBC kulifanya idadi kubwa ya wapiga kura kutoshiriki zoezi hilo.

Walisema mivutano baina ya makamishna wa IEBC na mwenyekiti wao ilichangia kupoozesha zoezi za uchaguzi huo wa marudio.

Aidha Mwau aliambia mahakama hiyo kwamba kutofanywa upya kwa uteuzi wa wagombea urais kulifanya uchaguzi wa Rais Uhuru Kenyatta kutotambulikana kisheria.

Sababu nyingine iliyotolewa ni kujitokeza kwa asilimia ndogo ya wapigakura na uchaguzi kutofanyika maeneo yote 290 ya uwakilishi bungeni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles