24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

MAMA UWOYA AKESHA AKIMUOMBEA NDIKUMANA

Na KYALAA SEHEYE

MAMA mzazi wa msanii, Irene Uwoya, Naima Uwoya, usiku wa kuamkia jana amekesha akimuombea aliyekuwa mkwewe Hamad Ndikumana, katika Kanisa Katoliki Mbezi Jogoo, Dar es Salaam.

Maombi hayo ni kwa ajili ya kumtaka apunguziwe adhabu ya kaburi na wao kumshukuru Mungu ili aweze kuondoa simanzi ndani ya moyo wake ikiambatana na msamaha.

Akizungumza na MTANZANIA, Mama Uwoya alisema siku zote za uhai wake hataacha kulitaja jina la mkewe katika maombi  kwa kuwa anaamini angeanza yeye, marehemu Ndikumana angefanya hivyo kwa jinsi walivyoishi kwa kupendana na kuheshimiana.

“Sitaacha kumuombea marehemu mkwe wangu hadi siku naingia kaburini, nitaomba sana ili apumzike kwa amani hata kama ana kinyongo na familia yangu, tulimpenda familia nzima na naamini hata vizazi vyetu vijavyo vitampenda kwa kusikia matendo yake,” alisema mama Uwoya.

Alisema atahakikisha anampa faraja mzazi mwenziye (mama Ndikumana), kwa kuongea naye mara kwa mara kama alivyokuwa akiongea na marehemu na kumpelekea mjukuu wake ili amzoee na wajisike faraja ya kumuona mwanaye kupitia Krish.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles