24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

WASANII KUFUNIKANA FIESTA DAR

Na MWANDISHI WETU

NI miezi takribani mitatu tangu kuzinduliwa kwa tamasha la burudani la Tigo Fiesta 2017, katika Uwanja Sheikh Amri Abeid, Arusha, kwa wasanii mbalimbali wa muziki wa Bongo Fleva kuanza ziara ya kimuziki katika mikoa 15 ya Tanzania Bara.

Shangwe za burudani za Tigo Fiesta 2017 ikiwa na kaulimbiu ya ‘Tumekusoma’, ilianza katika Jiji la Arusha Septemba 9 na kuzunguka mikoa ya Kahama, Mwanza, Mbeya, Singida, Kilimanjaro, Kigoma, Tabora, Mara, Ruvuma, Njombe, Dodoma, Tanga, Iringa, Morogoro na Mtwara.

Mashabiki wa mikoa hiyo walipata burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wanaowapenda kama vile Ali Kiba, Aslay, Ben Pol, Vanessa Mdee, Chege, Lulu Diva, Nandy, Rostam, Madee, Darassa, Jux na wengineo.

Sasa ni zamu ya Dar es Salaam kushuhudia wasanii wao wakali wanaowapenda Novemba 25, mwaka huu katika viwanja vya Leaders Club, wakiwapa raha ya kufunga tamasha hilo la Tigo Fiesta.

Mashabiki wa burudani wanasubiri kuona wasanii mbalimbali wakifunikana katika tamasha hilo, baada ya kufanya hivyo katika mikoa hiyo.

Meneja Masoko wa Tigo, William Mpinga, amesema tamasha la Dar es Salaam litakuwa la aina yake na mashabiki watarajie burudani kabambe kutoka kwa wasanii wakali ambao wanafanya vizuri katika muziki wa Bongo Fleva nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles