23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MREMBO WA TANZANIA AINGIA ‘TOP 20’ MISS WORLD

Na CHRISTOHER MSEKENA

SHINDANO la urembo la dunia, Miss World linatarajia kufanyika kesho huko Sanya China na Tanzania ikiwakilishwa na mrembo, Julitha Kabete ambaye amefanikiwa kuingia kwenye ‘Top 20’ ya warembo wanaofanya shughuli zenye tija kwenye jamii (Beauty with a Purpose), zinazohusu mabadiliko ya hali ya hewa.

Julitha Kabete amefanikiwa kuingia kwenye orodha hiyo kupitia makala yake fupi inayohusu jalala la Pugu Kinyamwezi lililopo Ilala, Dar es Salaam na anashindana na warembo wengine kutoka nchi 19.

“Namshukuru Mungu Tanzania imeingia Semifinals Top 20 Beauty with a Purpose. Naomba tuendelee ‘ku-like’ picha za Miss World, ‘Likes’ zinahesabiwa sana hasa muda huu ambao tumebaki na siku 1 tu,” aliandika Julitha Kabete katika ukurasa wake wa Instagram akiwataka Watanzania kuendelea kuzipenda (Like) picha zake kwenye mitandao ya kijamii ili aweze kushinda kwenye kipengele hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles