23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

MADIWANI WAASWA KUACHA USANII

Na PETER FABIAN

MADIWANI wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Wilaya ya Nyamagana   wametakiwa kuacha usanii wa kuendekeza mgogoro     baina yao na  Meya wa Jiji hilo, James Bwire pamoja na Mkurugenzi,  Kiomoni Kibamba.

Wametakiwa kuacha  kutumia fedha za walipakodi kujilipa posho bila kufanya vikao vyenye tija  kuwaletea maendeleo wananchi.

Ushauri huo ulitolewa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na jumuiya zake  za kata na Tawi la Mahina.

Wamewataka madiwani kuacha  kuzua migogoro inayokwamisha maendeleo ya wananchi   waliowachagua kuwatumikia.

Walikuwa wakizungumza na waandishi wa habari jana   wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Kata hiyo, Felician Burakari.

Nurakari alisema  mgogoro unaoendelea kwenye halmashauri Jiji kati ya Meya, Mkurugenzi na madiwani unaidhoofisha CCM na kudumaza maendeleo ya wananchi .

“Tukerwa na minyukano ya siasa kati ya Diwani wetu, James Bwire  ambaye ni  Meya wa Jiji na Mkurugenzi Kiomoni Kibamba na baadhi ya madiwani.

“Migogoro yao  wasiilete katika kata yetu, wao wanyukanie kwenye ofisi za halmashauri  lakini pia wakumbuke kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa vitendo,” alisema Burakari.

Alisema  madiwani na maofisa wa halmashauri ya jiji walikwenda kwenye kata hiyo kutembelea eneo inakojengwa hospitali na Kampuni ya Nyamwaga Ltd inayomiliki Kituo cha Alliance Sports Academy bila kutoa taarifa kwa uongozi wa serikali ya mtaa, kata na wamiliki wa eneo hilo.

Burakari alisema hatua hiyo ilisababisha watimuliwe kwa mawe na wananchi.

“ Madiwani na maofisa wa jiji (wataalamu)  walifuata nini bila taarifa kukagua mradi ambao  hauhusiani na  jiji  ? huku wakijua kuwa eneo hilo ni mali ya Kampuni ya Nyamwaga na Alliance Sports Academy ambayo ina uongozi wake.

“Eneo hilo  lilinuliwa kutoka kwa wamiliki wa asili na halikuwahi kulipwa fidia, na jiji  wakijua  kuwa mgogoro wa eneo hilo uko mahakamani?” alihoji Burakari.

Katibu wa CCM Tawi la Mahina, Prudence Gabriel, aliyekamatwa pamoja na Burakari, alisema madiwani hawana budi waache usanii kwa sababu  muda huo umeisha umebaki wa kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Viongozi wa CCM Burakari na Gabriel walikamatwa na polisi Novemba 9, mwaka huu wakiwa kwenye kampeni za udiwani katika Kata ya Mhandu.

Walidaiwa  kuwashambulia madiwani na maofisa Jiji la Mwanza waliokwenda kwenye eneo lenye mgogogro uliopo baina ya halmashauri na Kampuni ya Nyamwaga ambayo meya ni mmoja wa wakurugenzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles