Majosho ya mifugo yajengwa makazi, masoko Manyara

0
515

Mohamed Hamad, Babati

Majosho ya kuogeshea mifugo mkoani Manyara yanadaiwa kuvamiwa na wananchi na kujenga makazi na masoko.

Hayo yamebainika katika ziara ya kutathmini majosho yaliyopo nchini, ambapo akizungumza na Mtanzania Digital, Daktari Mkuu wa Mifugo mkoani humo, Dk. Christine Bakunambi,
amesema hali hiyo imechangia vifo vingi vya mifugo nchini kutokana na ugonjwa wa kupe.

“Majosho yamevaniwa katika maeneo tofauti, yamejengwa masoko na mengine makazi ya kuishi watu, hivyo hayawezi kutumika kwa sababu yalipaswa kuwa na maeneo ya kutosha, kwanza kukusanya mifugo na kujengwa birika la maji ya mifugo kabla ya kuogeshwa,” amesema.

Aidha, Dk. Bakunambi ametoa wito kwa halmashauri nchini, kutenga maeneo ya kutosha ya kuogeshea kama sheria za mifugo zinavyoelekeza.

Kauli hiyo inaakisi hatua ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, hivi karibuni kuzindua uogeshaji wa mifugo huko Chato mkoani Geita, akisisitiza mapambano na adui wa mifugo kupe yaendelee kwa kuogesha mifugo hiyo.

Katika uzinduzi huo, Serikali imegawa bure dawa kwa wafugaji na kuagiza kuundwa haraka kamati za kusimamia zoezi hilo ambapo awali zilikuw zikisimamia na baadaye kulegalega.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here