25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

MAGUFULI ASISITIZA USHIRIKIANO TANZANIA, UGANDA

 

|Anna Potinus, Dar es Salaam



Rais John Magufuli amesema Tanzania na Uganda zitaendelea kufanya biashara kwa pamoja ili kuimarisha uchumi wa nchi zote mbili na kudumisha mshikamano kati yao.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Agosti 9, Ikulu jijini Dar es Salaam wakati Rais Magufuli akizungumza baada ya mazungumzo yake na  Rais Yoweri Museven ambaye aliambatana na viongozi mbalimbali kutoka nchini Uganda.

“Nimefurahia sana ziara ya mzee wetu Museven pamoja na ujumbe aliokuja nao hivyo ningependa Tanzania na Uganda tufanye biashara kwa pamoja na tuwe kama ndugu,” amesema Magufuli

Aidha rais Magufuli amesema wamekaa na Rais Museven na kukubaliana kutafuta namna ya kuzuia watu wenye lengo la kuharibu viwanda vya Uganda kutokana na hali hiyo kuwahi kutokea kipindi cha nyuma

“Kuna sukari iliwahi kuingizwa hapa nchini kumbe ilikuwa haijatengenezwa na viwanda vya Uganda bali ilikua na lengo la kuharibu viwanda vyao hivyo tumezungumza na rais Museven ili suala hilo lisijitokeze tena,” amesema Rais Magufuli

Rais Museven yupo nchini kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuimarisha ushirikiano na ujirani mwema uliopo kati ya Tanzania na Uganda.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles