21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

AFRICAN LYON YASHUSHA KOCHA NA STRAIKA MFARANSA

NA LULU RINGO


TIMU iliyopanda daraja kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2018/19, African Lyon leo imemtambulisha kocha na mchezaji wote raia wa Ufaransa kwa lengo la kusaidia timu hiyo ifanye vizuri kwenye ligi hiyo.

Kocha huyo mpya anayetambulika kwa jina la Soccoia Lionel na mchezaji anayetambulika kwa jina la Victor Dacosta wote kwa pamoja wameingia mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo.

Kocha huyo aliyewahi kuifundisha AFAD ya Ivory Cost, CIFAS ya Benin na Cotton Spots ya Gabon amesema amejiandaa vizuri kupambana na ligi kuu ya nchini Tanzania na anaimani timu yake itafanya vizuri.

Naye Victor Dacosta aliyeonekana kuwa na furaha mno amesema ndoto yake ya muda mrefu ilikuwa ni kucheza Ligi Kuu ya Tanzania. “Naipenda Tanzania tangu nikiwa mdogo ina mazingira mazuri na hali ya hewa nzuri tamaa yangu kwa muda ilikua kucheza Ligi Kuu nchini Tanzania, kwasasa nina furaha sana” Alisema Victor.

Naye Meneja wa timu hiyo, Adam Kipatacho amesema timu hiyo imefanya usajili mzuri japo watu wengi wanatizama usajili wa vilabu vyenye majina makubwa tu na kusahau timu zenye majina madogo kama timu yake.
“Wengi wanatizama usajili wa timu kubwa, lakini katika timu zilizofanya usajili mzuri basi African Lyon ni mojawapo,” alisisitiza Meneja huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,654FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles