25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Magari ya mizigo yawekewa masharti kudhibiti corona

Ramadhan Hassan -Dodoma

MAWAZIRI sita wa afya wa nchi za Afrika Mashariki, wameweka masharti kwenye kila gari la mizigo madereva wasizidi watatu wakati wakivuka mipaka ya nchi hizo ili kukabiliana na kusambaa virusi vya corona.

Hayo yalielezwa jana jijini hapa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Ummy alisema mawaziri wa afya, ujenzi, biashara na ulinzi wa nchi sita wa Afrika Mashariki juzi walifanya mkutano kwa njia ya video conference na kukubiliana mambo kadhaa ikiwemo kuwaelekeza mawaziri wa afya wa nchi hizo kuweka masharti kwenye magari ya mizigo.

Alisema wamekubaliana usafirishaji wa bidhaa na huduma ndani ya Afrika Mashariki kuweka masharti kwamba kwenye gari la mizigo wasizidi watu watatu kuvuka mpaka.

“Tumeweka masharti kwamba kwenye gari la mizigo wasizidi watu watatu kuvuka mpaka, tumekubaliana hawa watatu watakuwa katika ukaguzi na endapo watagundulika wana maambukizi hilo gari litazuiwa kabla ya kuendelea na safari,” alisema Ummy.

Pia wamekubaliana mara baada ya wageni wanaoingia katika nchi zao kukaa karantini kwa siku 14, pindi wanapoondoka wapimwe tena ili kuonekana kama wana maambukizi ya ugonjwa wa corona.

“Tumekubaliana kuwekwa siku 14 kwa watu wote wanaokuja katika ukanda wetu. Jingine jipya kubwa, tutakuwa tunawakagua hata wageni ambao watakuwa wanaondoka,” alisema Ummy.

Aidha, alisema wameielekeza Tume ya Utafiti ya Afrika Mashariki  kufanya utafiti kuhusu dawa, chanjo, wagonjwa na masuala ya sera.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles