24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Madiwani Lindi waichongea halmashauri yao kwa kutowalipia NHIF

Hadija Omary, Lindi   



Hatua ya Halmashauri ya Manispaa ya Lindi mkoani humo kutowasilisha michango kwenye Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), kimesababisha madiwani wa halmashauri hiyo kushindwa kutumia kadi zao za  mfuko huo wanapokwenda kupata matibabu katika hospitali mbalimbali kwa zaidi ya miezi tisa.

Suala hilo limeibuliwa leo katika kikao maalumu cha Baraza la Madiwani la Manispaa hiyo cha kupitia taarifa ya mahesabu ya mwisho 2017/18.

Wakiwasilisha malalamiko yao baadhi ya madiwani hao wamesema licha ya kuwepo na makato ya kila mwezi kwa ajili ya kulipia huduma hiyo lakini bado wanapokwenda kupata huduma ya matibabu wanashindwa kutumia kadi zao kwa kile kinachodaiwa kuwa kadi hizo zimefungiwa.

“Changamoto kubwa ni pale tunapoambiwa kadi haziwezi kutumika kwa sababu kadi hizo hazijalipiwa hivyo inatulazimu kutumia fedha taslimu ili kupata huduma.

“Kwa mfano Julai nilimpeleka baba yangu mzazi kutibiwa katika Hospitali ya Brigita ila alipofika pale aliambiwa huwezi kupata huduma nilipofuatilia katika ofisi za Bima ya Afya niliambiwa kuwa halmashahuri yetu haijafikisha malipo yetu ya mchango tangu mwezi Januari mwaka huu lakini hata niliporudi halmashahuri ili kupata ufafanuzi zaidi mkurugenzi alikiri kweli kuna deni bima ya afya lakini ni la miaka ya nyuma,” amesema Diwani wa Kata ya Mwenge, Ahmad Zuberi.

Kutokana na hali hiyo, Naibu Meya wa Manispaa ya Lindi, Hasina Kawanga ametoa mwezi mmoja kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha inalipa deni hilo ili madiwani waweze kupata huduma kwa kutumia kadi hizo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi Baptista kihanza alisema kuwa ni kweli halmashauri yao inadaiwa na NHIF Sh milioni nane   ambayo ilikuwa ni malimbikizo ya deni la madiwani wa Baraza la Madiwani la mwaka 2013/14 na kuhaidi kulilipa deni hilo kwa kadri halmashauri itakapopata fedha kutoka katika makusanyo yake ya ndani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles