Imechapishwa: Mon, Jun 4th, 2018

Licha ya majeraha Vicent Kompany aitwa kikosi cha Ubelgiji

 

BRUSSELS, Ubelgiji
BEKI wa kutumainiwa wa Manchester City na nahodha wa Timu ya Taifa ya Ubelgiji, Vincent Kompany amejumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 23 watakaoiwakilisha nchi hiyo kwenye Kombe la Dunia litakalofayika nchini Urusi licha ya kupata majereha kwenye mechi ya kirafiki iliyochezwa Jumamosi iliyopita.
Vicent Kampany alipata majeraha hayo wakati wa mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Ureno.
Kocha wa Ubelgiji Roberto Martinez alisema Kompany alihisi wasiwasi wakati alipopata majeraha hayo lakini hata hivyo amejumuishwa kutokana na jereha lake kutokuwa na madhara makubwa kushindwa kuiwakilisha nchi yake kulisaka kombe hilo.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

Licha ya majeraha Vicent Kompany aitwa kikosi cha Ubelgiji