23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

KHLOE KARDASHIAN: SIKUWA NA UJANJA KUZUIA UJAUZITO

NEW YORK, MARAKENI

MDOGO wake Kim Kardashian, mwanamitindo Khloe Kardashian, amefunguka kwa mara ya kwanza juu ya ujauzito wake na kusema hakuwa na ujanja wa kuzuia kupata mimba kipindi hiki.

Mrembo huyo amesema baada ya kuanza uhusiano na mpenzi wake Tristan Thompson, ambaye ni nyota wa kikapu wa Ligi ya NBA nchini humo katika timu ya Cleveland Cavaliers, alimwambia hasitumie kinga yoyote ya mimba kwa miezi sita.

“Nilikuwa najua njia nyingi za kuzuia ujauzito, lakini kwa sasa siwezi kuzifikiria tena kwa kuwa tayari nimeamua kuja kuitwa mama hivi karibuni na mpenzi wangu Tristan Thompson.

“Wakati tunaanza uhusiano mapema mwaka huu aliniambia niache kutumia kinga zote za ujauzito kwa miezi sita, ilikuwa ngumu kukubali, lakini kwa kuwa nampenda ilibidi nikubali yale asemayo, hivyo nilikubali na matokeo yake yamekuwa vile alivyotarajia,” alisema Khloe.

Hata hivyo mapema mwakani familia ya Kardashian inatarajia kuongeza watoto huku ikiwa aliyekuwa mpenzi wa Tyga, Kylie Jenner anatarajia mtoto na mpenzi wake wa sasa rapa Travis Scott.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles