24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 8, 2024

Contact us: [email protected]

BIFU LA P SQUARE, VYUMA VIMEKAZA

Na CHRISTOPHER MSEKENA

WAKATI  hapa Bongo tukiwa tumebakiwa na masalia ya Kundi la Yamoto Band, wiki hii kundi kutoka Nigeria linaloundwa na mapacha, Peter na Paul Okoye ‘P Square’ limeingia kwenye jaribio jingine la kuvunjika.

Mapema wiki hii mwanamitandao maarufu nchini Nigeria, Linda Ikeji kupitia blog yake alivujisha video inayowaonyesha ndugu hao wakiwa kwenye malumbano ambapo Paul (yule mwenye rasta) na kaka yao mkubwa  ambaye ni meneja wa kundi anayeitwa Jude wakimshambulia Peter.

Mara kadhaa Peter (yule anayenyoa nywele) amekuwa akihitaji kupewa nafasi ya kuendelea kufanya kazi zake binafsi nje ya kundi ambapo Jumatatu wiki hii alimwandikia barua ya kujitoa kundini mwanasheria wa kundi hilo, Festus Keyamo na kusambaza nakala zingine kwenye vyombo vya habari nchini humo.

Katika nakala ya barua hiyo, Peter ambaye hivi sasa anatambulika kwa jina la Mr P, alimtupia shutuma kadhaa pacha wake Paul kuwa hana utayari tena na moyo wa kushirikiana kwenye kazi kufuatia kutotokea kwenye ziara yao nchini Marekani pamoja na kuichafua familia yake yaani watoto wake (Cameron na Aliona) na mkewe kipenzi Lola Omotayo.

Kadhalika kwenye barua hiyo ya kujiondoa kwenye kundi la P Square, Mr P hakumwacha salama kaka yao mkubwa, Jude Okoye kwani alimtuhumu kuwa amewahi kutoa vitisho vya kumpiga risasi na kumuua mkewe jambo lililofanya afikie uamuzi wa kujiondoa.

 PAUL AKOLEZA BIFU

Katika kuonyesha kuwa bifu hilo siyo kiki, Peter Okoye alitumia ukurasa wake katika Mtandao wa Kijamii wa Snap Chat kuwa yupo nchini Uingereza kwa shoo yake binafsi bila pacha wake huyo na  aliandika hivyo baada ya Paul kutumia ukurasa wa Instagram kuandika maneno yaliyotafsiriwa kuwa anamsema shemeji yake yaani mke wa Peter ambaye amekuwa akimtuhumu kumpelekesha nduguye.

Paul aliandika: “Siku zote panapokuwa na amani mtu anayeiharibu amani ni mwanamke.”

WAKILI WAO AITULIZA JAMII

Mara baada ya Peter kuandika barua hiyo ya kujitoa kundini, mwanasheria wao Festus Keyamo alitoa maelezo yaliyoitaka jamii kutulia, kuwaombea na kuwapa nafasi ya faragha mapacha hao kujadili kile kilichotokea.

Amesema kuwa ni ugomvi wa kawaida, na si ajabu kutokea kwenye familia nyingi duniani. Wakili huyo aliweka wazi kuwa video iliyovuja Jumanne hii ikiwaonyesha mapacha hao wakigombana ni ya Mei, mwaka jana na kwamba ugomvi huo ulishamalizwa.

Festus amewataka Peter na Paul kutofanya mazungumzo na chombo chochote cha habari ili kuzuia kukuza ugomvi huo.

UKABILA, UMRI WAINGIA

Mke wa Peter, Lola amekuwa akituhumiwa kuwa chimbuko la ugomvi huo, huku baadhi ya mashabiki wao nchini humo wakihusisha masuala ya ukabila kuwa ni chanzo cha ugomvi huo.

Inafahamika kuwa mke wa Peter anatoka kabila la Yoruba huku Peter akiwa ni kabila la Igbo na suala la ukabila nchini Nigeria ni kitu kinachoangaliwa mno ndiyo maana Lola anatuhumiwa kuleta fitna kwenye ukoo wa Okoye kwa kuwa ni kabila tofauti.

Hata hivyo, wakili Festus amelikanusha na kuwatetea wake wa mapacha hao, Lola na Anitha kuwa wamekuwa mbali kabisa na ishu zinazohusiana na P Square.

Pia mke wa Peter (Lola) ana umri mkubwa, amemzidi Mr P miaka sita jambo linahusishwa kuwa chanzo cha Paul kuonyesha chuki za wazi kwa shemeji yake (mke wa Peter).

KILA MTU NA MICHONGO YAKE

Hivi sasa Peter ambaye hapa Bongo anafanya vyema kupitia wimbo wa Vanessa Mdee unaoitwa Kisela, amewekeza muda wake mwingi kwenye kazi zake binafsi kama vile kutangaza shoo zake, kuendesha shindano la Dance With Peter na michongo mingine inayompa pesa.

Upande wa Paul kwa muda mrefu sasa amekuwa akiambatana na kaka yake mkubwa, Jude huku akijitika zaidi kuendeleza studio yake Rude Boy Recordz na kutaka kulilinda Kundi la P Square lisimeguke.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles