23.6 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Kagera wahamasishwa kupima homa ya ini, HIV

Na RENATHA KIPAKA-BUKOBA

WANANCHI mkoani Kagera, wameshauriwa kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara hasa homa ya ini na virushi vya Ukimwi (HIV).

Ushauri huo ulitolewa na daktari wa kiwandacha sukari cha Kagera Sugar, Johanes Tinga, wakati wa kilele cha Sikukuu ya Wakulima – Nanenane, alipokuwa anaendesha upimaji afya bure katika banda lao, viwanja vya Kyakairabwa mjini Bukoba.

Dk. Tinga alisema kwa siku nane ambazo wamefanya upimaji bure, wananchi waliojitokeza wengi wao ni kina mama.

 “Ili mtu aishi salama, anatakiwa kupima afya yake mara kwa mara maana ni bora kinga kuliko tiba, sasa inasikitisha kuona wanawake ndio wanaojitokeza kupima afya zao na wakati wanaotakiwa kuwa mfano katika afya kwenye familia ni wote wawili,” alisema.

Dk. Tinga alisema katika maonyesho hayo, wananchi waliopima homa ya ini ni 100, sukari na presha 250 na waliopima HIV ni 150.

Alisema baadhi ya wananchi wamekuwa wagumu kupima ini na HIV kwa sababu ya kuogopa kupata majibu.

 “Ndugu zangu ugonjwa wa homa ya ini unatisha sana, pimeni mapema ili mpatiwe chanjo maana ukisubiri tatizo liwe kubwa kufanya matibabu, itakuwa haisaidii tena,” alisema Dk. Tinga.

Kwa upande wake Juma Joansen kutoka wilayani Muleba aliyefika kupima afya katika banda hilo, alisema kuwa kupima afya ni bora maana kupitia upimaji huo aligundua kuwa ana tatizo la presha ambalo hakuwa anajua.

“Mimi nilikuwa naugua mara kwa mara kichwa, wakati mwingine homa na mapigo ya moyo yalikuwa yanakwenda mbio, ila sikuwa naona umuhimu wa kupima.

“Sasa nimepima bure afya yangu, naanza kufuatilia huduma hospitali ili nielekezwe jinsi ya kuishi kwa usahihi,” alisema Joansen.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles