JPM AWATIA PRESHA VIGOGO

0
375

Na MWANDISHI WETU


ZIARA ya kikazi ya siku saba anayoifanya Rais Dk. John Magufuli katika mikoa ya Mwanza, Simuyu na Mara inaonekana kuwaweka katika wakati mgumu baadhi ya vigogo wa serikali.

Ziara hiyo ambayo Rais ameweka mawe ya msingi, kufungua miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi kupitia mikutano ya hadhara imekuwa mwiba kwa baadhi ya watendaji wa serikali.

Tayari baadhi ya watendaji  wametumbuliwa katika nyadhifa zao,  wengine kushikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi lakini pia wapo waliojikuta katika wakati mgumu wa kutoa ufafanuzi mbele yake juu ya hatua walizozichukua kutatua kero za wananchi.

Kinachoakisi kuwa ziara hiyo imeibua presha kwa vigogo wa serikali ni uamuzi wa ghafla wa Rais Magufuli kuwatumbua vigogo wawili wa juu serikalini.

Vigogo hao ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Valentino Mlowola  pamoja na Kamishna wa Ardhi Kanda ya Ziwa, ambaye Rais Magufuli alimtaja kwa jina moja tu la Chawio.

Akizungumzia sababu iliyomsukuma kumtumbua Mlowola, Rais Dk. Magufuli alisema pamoja na makosa mengine lakini kitendo cha Takukuru makao makuu kukalia faili  la uchunguzi wa mtu aliyenunua Musoma Hoteli ambayo imekaa miaka kumi bila kufanya kazi  wakati mtu huyo huyo ndiye anayepewa kandarasi za ujenzi wa barabara mkoani humo ni miongoni mwa sababu zilizoharakisha uamuzi wake huo.

 Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here