JPM atishia kufukuza wakurugenzi wakaidi

0
368

PENDO FUNDISHA-MBEYA

RAIS Dk. John Magufuri, ametangaza kuwafukuza kazi wakurugenzi wote wa halmashauri ambao watabainika kukiuka sheria ya ufutaji wa tozo za ushuru wa mazao.

Alisema baada ya kuingia madarakani, Serikali iliondoa tozo 80, miongoni mwa hizo tozo ushuru wakulima ambao walikuwa wakilipa mazao kutoka halmashauri moja kwenda nyingine.

Rais Dk. Magufuli, aliyasema hayo juzi alipokuwa akiwahutubia wakazi wa Wilaya ya Kyela katika ziara ya kikazi ya siku 10 mkoani Mbeya.

Alisema, sheria ya ufutaji wa tozo hizo zilipitishwa na Bunge hivyo hakuna mtu yoyote wa kuitengua na kwamba Mkurugenzi atakaye itengua atakuwa umevunja sheria na anawajibu wa kufukuzwa kazi.

Alisema licha ya kupitishwa kwa sheria hiyo wapo baadhi ya watendaji wameendelea kuwatoza ushuru wananchi kwa kisingizio cha kupandisha ukusanyaji wa mapato hilo jambo sitaki kulisikia.

“Wapo watendaji wanasema kufutwa kwa ushuru kunapunguza mapato, narudia kwa viongozi wote, wakurugenzi, watendaji wote wa halmashauri msiwatoze wananchi ushuru wa mzigo wowote usio zidi tani moja,”alisema.

Hata hivyo, alitoa wito kwa watendaji kuzingatia sheria ya kuwalinda wakulima na ndio maana serikali iliziondoa tozo 80.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here