JPM AAGIZA TAKUKURU IFUMULIWE

0
732
KIAPO: Rais Dk. John Magufuli akimuapisha Kamishna Diwani Athuman Msuya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa nchini (TAKUKURU), Ikulu ya Chamwino Dodoma jana. Picha na Ikulu

Na MWANDISHI WETU – DODOMA


RAIS Dk. John Magufuli amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Kamishna wa Polisi (CP) Diwani Athumani, kufumua muundo wa taasisi hiyo ili watendaji wanaojihusisha na rushwa wachukuliwe hatua.

Alitoa kauli hiyo jijini hapa jana baada ya kumwapisha CP Athumani kuwa mkurugenzi mpya wa Takukuru ikiwa ni siku chache tangu atengue uteuzi wa Valentino Mlowola aliyekuwa bosi wa taasisi hiyo.

Wiki iliyopita, Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Mlowola huku akieleza sababu ya uamuzi wake huo kuwa ni pamoja na taasisi hiyo kutoshughulikia vitendo vya rushwa mkoani Mara.

“Nimekwenda pale Musoma mtu amenunua Musoma Hotel kwa miaka kumi hashughuliki, anapewa kazi za kandarasi hamalizi. Waziri Mkuu alipita hapa Mara akatoa maagizo kwa Takukuru kwamba washughulikie.

“Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mara alilishughulikia na akamaliza tangu mwezi wa nne na akapeleka faili makao makuu, lakini hadi leo mwezi wa tisa makao makuu bado hawajalishughulikia,” alisema.

Alisema makao makuu kulikalia faili hilo ndiyo sababu iliyomfanya aone kuwa Mlowola lazima akae pembeni akafanye kazi nyingine.

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here