23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Jaguar akamatwa na polisi


Nairobi, Kenya

Mbunge wa Jimbo la Starehe nchini Kenya Charles Njagua maarufu Jaguar amekamatwa nje ya ukumbi wa Bunge la nchi hiyo na amepelekwa kituo cha polisi, amekamatawa baada ya kutoa kauli za chuki za kuwataka Watanzania na raia wa nchi nyingine waishio nchini humo kuondoka.

Jaguar amekamatwa leo Jumatano Juni 26, saa 6:30 mchana na polisi waliokuwa wamevalia mavazi ya kiraia waliokuwa wanamsubiria katika gari ya nje ya bunge hilo.

Mbunge huyo ambaye pia ni mwanamuziki amekamatwa baada ya kutoa kauli za kibaguzi kwa raia wa Tanzania na nchi nyingine alipokuwa akihutubia wafanyabiashara katika barabara ya Kirinyaga jijini Nairobi akisema raia wa kigeni wamechukua maeneo mengi ya nchi hiyo hivyo wanapaswa kuondoka ama watawaondoa kwa lazima.

Jaguar alionekana akisema “Tunaongea juu ya mamia wanaotoka nchi za nje kuja kufanyakazi hapa (Kenya), nataka niseme leo natoa saa 24 kama hao watu hawatarudi kwao mimi kama mbunge wa hapa tutaingia kwenye maduka wanayofanyia kazi, tutawatoa, tutawapiga na tutawapeleka Airport (uwanja wa ndege).

“Kazi ya immagration (Uhamiaji) itakua kuwachukua uwanja wa ndege kuwapeleka kwao, tumekuwa na kesi hapa leo, mtu kutoka nje anafanya biashara hapa, imefika mahali wanakuja kuwasumbua hapa nchini kwetu, sisi kama wananchi wa Kenya na wafanyabiashara wa hapa, hatutasubiri watu kutoka nje kuja kuharibu biashara za Wakenya hapa.

Huku akishangiliwa na wafuasi wake, aliongeza: “Ukiangalia kwenye magari Wapakistani, Wachina wamechukua biashara, Masokoni Watanzania na Waganda wamechukua hizo biashara sasa tumesema inatosha, kama tukiwapa saa 24 na hawajatolewa hapa, sisi tutawatoa, tutawapiga na hatuwaogopi.”

Hata hivyo, tayari serikali ya Kenya imekanusha kuhusika na kauli aliyoitoa Mbunge huyo ikisema kauli hiyo haina nafasi katika mazingira ya dunia ya sasa huku bunge likiahidi kumchukulia hatua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles