24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

HUKU JUX NA VANESSA, KULE DIAMOND NA ZARI…

  • Ni penzi la dhati au kikazi zaidi?

Na JOSEPH SHALUWA

KAPO za mastaa duniani kote zimekuwa na utata. Aina ya maisha yao pia ni sababu nyingine inayowafanya kila kitu kinachoendelea kwenye maisha yao kijulikane kwa jamii.

Hapa Bongo kapo zinazotikisa zaidi ni za wanamuziki maarufu wa Bongo Fleva, Juma Jux na Vanessa Mdee ‘V Money’, mwanamuziki wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mjasiriamali kutoka Uganda, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’.

Vanessa na Jux kuna wakati walizinguana na uhusiano wao ulivunjika rasmi, kila mmoja akaendelea na maisha yake. Hilo ni tukio la muda kidogo, lakini hivi karibuni tukio la Diamond kukiri kuzaa na mwanamitindo Hamisa Mobetto limeibua mushkeli kwenye penzi lake na Zari.

Lakini wikiendi iliyopita, Zari aliingia nchini akitokea Afrika Kusini anapoishi, kisha akaonekana kufanya matanuzi na Diamond visiwani Unguja, Zanzibar. Kabla ya hapo alikuwa kwenye uzinduzi wa duka la Danube Home, lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam.

TUANZE NA DIAMOND

Diamond Platnumz aliyekuwa na shoo katika Viwanja vya Amaan mjini Unguja wikiendi iliyopita Oktoba 14, mwaka huu aliongozana na mzazi mwenzake Zari, jambo lililoonyesha kuwa hapakuwa na bifu tena kati yao.

Wawili hao waliungana pamoja baada ya Diamond kutua Bongo akitokea Miami, Florida nchini Marekani alipokwenda kwa ajili ya Tuzo za AFRIMMA na kukamilisha kolabo yake na Rick Ross.

Diamond na Zari waligeuka kivutio katika mitaa mbalimbali mjini Unguja. Maeneo kama Forodhani wanakuoza kalimati, urojo na mishikaki walishuhudia kapo hiyo matata.

Jumamosi ya Oktoba 14, katika onyesho hilo Chibu alitumia mgogoro wake na wapenzi wake (Zari na Hamisa) kupendezesha onyesho hilo. Hakusita kumtupia dongo Mobetto na kumsifia mama Tiffah (Zari).

Alitumia usanii kutengeneza stori ambayo iliendana na mtiririko mzuri wa nyimbo alizotumbuiza. Akiwa jukwaani katikati ya wimbo, Diamond alitoa break na kuanza kusimulia kisa cha mgogoro wake na Zari.

Katika maelezo hayo ya Diamond akiwa jukwaani alithibitisha kwamba alikuwa ameshaelewana na mpenzi wake Zari baada ya kumuomba msamaha kwa yaliyotokea.

“Unajua hapa katikati hapa yalitokea mambo mambo mengi, shetani aliingia katikati, mara ooh! Hivi na vile… ebwana mambo yakawa mengi unajua… nikaona eeenheee! Mtoto wa Kiganda kacharuka.

“Nikaangalia kushoto na kulia nikaona kabisa kama jiko naelekea kulikosa moja kwa moja. Nikala pipa nikaruka mpaka Sauzi. Nilifikia chumbani moja kwa moja… nikajua basi mambo ndiyo yatakuwa yameisha.

“Mambo yakaendelea. Niliporudi Tanzania nikaona mambo yamefunguka mengine… ametupa dongo Instagram, nikaona ohoooo! Nikapiga simu saa nzima nambembeleza lakini wapi. Nikamwambia mimi nimeteleza, mdudu ibilisi hapa amepita kati… akawa bado haelewi. Basi ukanijia wimbo kwenye kichwa,” alisema Diamond wakati jukwaani.

Baada ya maneno hayo, akaanza kuimba wimbo huo ‘Mwenzenu Basi’ huku mashabiki wakimsindikiza.

Kwa tafsiri rahisi ni kwamba Diamond na Zari tayari wameshaelewa na maisha yanaendelea ingawa yanayoendelea ndani mwao ni siri yao wenyewe.

Je, ni kweli wameshaelewana na hakuna ‘usanii’ unaoendelea kati yao? Ujio wa Zari Bongo ulikuwa kwa ajili ya mpenzi wake Diamond au ufunguzi wa duka la Danube kama balozi wake?

Je, Diamond alikuwa na mpango wa kuongozana na mpenzi wake huyo Zanzibar au aliamua kwenda naye hata kama wana bifu ili kunogesha onyesho lake visiwani humo? Hayo ni maswali yanayofikirisha ambayo wenye majibu sahihi ni wao wenyewe.

JUX, VANESSA

Hawa waliachana kwa maneno mengi, lakini juzi kati wamekuwa pamoja kwenye maonyesho ya Tigo Fiesta 2017 katika  mikoa mbalimbali nchini.

Bado haijajulikana kama ni kweli wawili hao wamerudiana kweli na siyo ‘kiini macho’ kama wengi wanavyofikiri huku wengine wakienda mbali zaidi na kuhusisha biashara ya wao  kupanda kwenye shoo za Fiesta huenda ndiyo iliyowakutanisha na kutengeneza drama kwa mashabiki.

Hata hivyo, Jux mwenyewe amewahi kukaririwa na mtandao mmoja hivi karibuni akisema amerudiana na Vanessa na kati ya jambo analotamani kwa sasa ni kuzaa na mpenzi wake huyo.

Gumzo kubwa liliibuka kwenye shoo ya jijini Mbeya iliyopewa jina la Tigo Fiesta Classic Mbeya ambapo walipanda jukwaani na kuimba pamoja kwa hisia kisha mwishoni wakamaliza kwa kukumbatiana, shangwe ikaibuka kwa mashabiki.

Ni shoo za Fiesta ndizo zimewakutanisha na kutengeneza drama kwa mashabiki au ni kweli penzi lao limerejea? Ukweli upo uvunguni mwa mioyo yao.

Yetu siye macho, ingawa maombi yetu ni uhusiano wao (Diamond na Zari, Jux na Vanessa) uwe wenye afya na ikiwezekana utengeneze ndoa hapo baadaye.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles