Imechapishwa: Sat, Oct 15th, 2016

Gobole, bangi zamkamatisha diwani, mkewe

bangi

Na Walter Mguluchuma- Sumbawanga

JESHI la Polisi Mkoa wa Rukwa linamshikilia Diwani wa Kata ya Izia (Chadema), Pascal Silwimba (41) na  mkewe Dorisi Karugu (36) kwa kukutwa na gobole na robo kilo za dawa za kulevya aina ya bangi wakiwa wamehifadhi ndani ya duka lao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando, aliwaambia waandishi wa habari mjini hapa jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa tatu asubuhi katika eneo la Soko Kuu la Manispaa ya Sumbawanga.

Alisema Pascal na mkewe walikamatwa  kutokana na msako walioufanya baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa watu hao wanamiliki silaha kinyume cha sheria na pia wamekuwa wakijihusisha na biashara ya kuuza bangi.

Kyando alisema baada ya taarifa hizo kuwafikia walianza kufanya uchunguzi  kuhusiana na tuhuma hizo na baada ya  uchunguzi kufanyika waliamua kufanya  msako katika eneo hilo.

Alisema baada ya kufanya uchunguzi huo, walifika dukani kwa Pascal na walipekua ndani ya duka hilo walilokuwa wakiuza mifuko ya salfeti na walikuta gobole hilo na bangi zikiwa zimehifadhiwa katikati ya mifuko hiyo.

Alisema baada ya kukamatwa na vitu  hivyo dukani mwao walihojiwa na kukiri   kuvimiliki. Kyando alisema upelelezi wa tukio hilo umekamilika na watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani ili sheria  ichukue mkondo wake.

Displaying 1 Amechangia
Toa Maoni Yako
  1. twaha salum says:

    HONGERA TASAF KUTOWA MALIPO KWA MTANDAO.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

FACEBOOK

YOUTUBE

Translate »

Gobole, bangi zamkamatisha diwani, mkewe