Ferguson awapa ubingwa Liverpool

0
693

LIVERPOOL, ENGLAND

KOCHA wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, anaamini klabu ya Liverpool ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa msimu huu dhidi ya wapinzani wao Manchester City.

Kocha huyo anaamini hivyo huku akidai Manchester City wanaweza kuja kupoteza mchezo wao dhidi ya Manchester United, ambapo timu hizo zitakuja kukutana kwenye Uwanja wa Old Trafford, Aprili 24.

Ferguson alifanya mazungumzo na baadhi ya wachezaji wa Burnley, Phil Bardsley na kumwambia kwamba United wana nafasi kubwa ya kushinda katika mchezo huo, hivyo wakishinda watawapa nafasi Liverpool.

“Ferguson ametuambia kwamba, Liverpool wana nafasi kubwa ya kuwa mabingwa msimu huu kwa kuwa Manchester City wanaweza kuja kupoteza mchezo wao dhidi ya Manchester United, hivyo itawapa nafasi Liverpool ya kuwa mabingwa,” alisema Bardsley.

Kwa sasa Liverpool wanaongoza kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 85 huku Manchester City wakishika nafasi ya pili wakiwa na pointi 83, lakini wapo nyuma kwa mchezo mmoja, hivyo timu hizo mbili zinapambana kushinda michezo yao yote iliyobaki, huku kila mmoja akimuombea mwenzake apoteze angalau mchezo mmoja, lakini City wakishinda michezo yote iliyobaki anakuwa bingwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here