23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Slaa, polisi wapambana Dar

slaaNa Faraja asinde, Dar es salaam,

HALI ya tafrani ilizuka jijini Dar es Salaam jana, baina ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa na askari wa Jeshi la Polisi.
Hali hiyo ilijitokeza, baada ya askari polisi kumhoji kiongozi huyo wa chama kikuu cha upinzani nchini, hatua yake ya kufanya mkutano bila kibali.
Tafrani hiyo ambayo iliibuka katika eneo la Tegeta Gereji ilianza saa 11:50 jioni baada ya Dk. Slaa kuwasili katika eneo hilo na kuanza kuhutubia ambapo wananchi walitoa malalamiko yao dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordani Rugimbana kwa kumilikisha eneo hilo kwa mwekezaji.
Akizungumza baada ya wananchi kuwasilisha malalamiko yao, Dk. Slaa alisema kwa muda mrefu Watanzania wamekuwa wakitenganishwa na vyama ila linapojitokeza suala lenye maslahi kwa Taifa huwa wanaondoa itikadi zao.
“Haiwezekani Serikali iwakabidhi eneo alafu leo iwaondoe ni jambo ambalo halikubaliki kwani mwekezaji mmoja hawezi kuwa na manufaa kushinda watu 4000.
“… lakini pia biashara ya magari inahitaji sehemu kuliko na magari sasa wakiwahamisha hapa na kuwapeleka huko wanakosema kazi zenu mtafanyaje inatakiwa mshikamane kwenye hili mwache woga.
“Mimi nitawasaidia mkionyesha jitihada kwani nalipwa ruzuku kutokana na kodi zenu hivyo nipotayari kuwapigania hivyo jumatatu nitatoa mawakili kwa ajili ya kupitia agizo hili kwani huwezi kumwacha mwananchi anaondolewa kwenye eneo hili naomba sasa mtambue kuwa kama ni ukombozi sasa umeanza,” alisema Dk Slaa.
Ilipotimu saa 11:40 jioni polisi walivamia eneo hilo, ambapo aaskari mmoja alkwenda katika jukwaa alilokuwa akihutubia Dk. Slaa na kutaka kumkamata hali iliyozusha malumbano makali kati ya wananchi na polisi
Dk Slaa alihoji kwa kusema: “Wewe ni nani, unataka nini na unatoka wapi? Polisi: Mimi natoka ofisi ya juu, ni nani aliyekupa kibali cha kufanya mkutano hapa?,” alihoji askari.
Kutokana na hoja hiyo Dk Slaa alijibu: “Kwani Kikwete anapofanya mkutano huwa anapewa kibali na nani?, si akijisikia tu anafanya?,” alihoji Dk. Slaa.
Mara baada ya majibizano hayo, wananchi waliokuwa wamekusanyika katika eneo hilo walianza kuzomea huku wakiwatuhumu askari polisi kuwa ndio imekuwa mazoea kwao kukamata watu.
Mkutano huo ulihudhuriwa na wenyeviti wa Serikali za Mitaa yote sita ya Kata Kunduchi wa CCM pamoja na wale wa Chadema.
MTANZANIA ilimtafuta Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana ili kuweza kupata ufafanuzi kuhusu madai hayo, ambapo alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwani kilichofanyika ni kusimamia agizo la mahakama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles