24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Dk.Bisimba anusurika kifo, avunjika mguu

Pg 1Na Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam

MKURUGENZI wa Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC), Dk. Hellen Kijo-Bisimba amenusurika kifo ajalini.

Dk. Kijo-Bisimba alipata ajali mbaya ya gari katika daraja  la Salender   Dar es Salaam jana.

Katika ajali hiyo, Dk. Kijo-Bisimba anadaiwa kuvunjika mguu mmoja baada ya gari lake kupoteza mwelekeo na kupinduka mara nne.

Ajali hiyo ilitokea  jana asubuhi wakati   akitoka kusali eneo la Posta   akitumia gari dogo   ya Toyota Prado   namba   T 159 ATY.

Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa LHRC, Ezekiel Masanja alisema baada ya kupata taarifa ya ajali hiyo   alikwenda   na kumchukua  Dk. Kijo-Bisimba.

Alisema alimpeleka katika Hospitali ya Agha Khan kwa   matibabu.

Masanja alisema vipimo vya awali vilionyesha amevunjika mguu  lakini  hadi jana jioni   madaktari walikuwa wakiendelea  kumuangalia zaidi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillus Wambura alikiri kutokea   tukio hilo akisema polisi wanaendelea  na uchunguzi wa ajali hiyo.

“Sina maelezo yanayojitokeza kuhusu ajali hii kwa sababu askari   wanaendelea kufanya uchunguzi  kujua chanzo chake,”alisema Wambura.

Mashuhuda   walisema gari la Dk. Kijo-Bisimba liligongwa   ubavuni na gari nyingine iliyokua inatoka   la Sea View kwenda barabara ya Ali Hassan Mwinyi.

Walisema gari hilo lilikua linaendeshwa na kijana ambaye hakufahamika na baada ya kuligonga gari la Kijo-Bisimba lilizunguka mara nne  na kupinduka.

Katika gari la Dk. Kijo-Bisimba walikuwamo watu wawili na inadaiwa gari lililomgonga lilikuwa likiendeshwa na kijana   wa miaka 13.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles