23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Bashiru awashukia waliohujumu TCCCO

Na Safina Sarwatt-Kilimanjaro

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM),kimesema hakitavumilia waliokihujumu kiwanda cha kukoboa Kahawa cha TCCCO kilichopo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro na kusababishia hasara ya mabilioni ya fedha kwa ununuzi wa mitambo mibovu.

Hayo yalisemwa mjini Moshi jana na Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally, alipotembelea kiwanda  hicho na kushuhudia madudu.

Alisema kufa kwa kiwanda hicho, ni hujuma haiwezekani viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia wapo wameridhika na hali hiyo.

Alisema mali za chama zimeuzwa na fedha hizo kutumika kwa ajili ya kununua mitambo mpya,bado mtambo huo haufanyikazi kwani ji jambo baya na la udanganyifu.

Alisema Serikali haitawavulia wale wote waliohusika wahusika kuhujumu kiwanda hicho.

“CCM haiwezi kuvumilia hujuma zinazofanya na baadhi ya viongozi wasiokuwa waadhili na waminifu na kwamba wahusika hao watachukuliwa hatua, kwani haliwezekani kiwanda kinakufa bila sababu .

“Si kwa kiwanda hiki tu, ni viwanda vyote vikubwa vya kimikakati vyote vimeuliwa na hao matapeli wasiokuwa na uchungu na nchi hii,watu wamekaa kiwizi wizi tu, kudokoa dokoa mali za umma,” alisema Dk. Bashiru

Alisema ndani ya Wizara ya Kilimo kuna tume ya ushirika, lakini bado hakuna wanachokifanya  kwani bado wizi na ubadhiorifu umekuwa ukiendelea katika usimamizi wa mali za umma.

“Mmegeuza uongozi kama jambo la kwenda sokoni,tunataka viongozi wenye uchungu na taifa hili. Waziri wa Viwanda Mei, mwaka huu alikuwa hapa alishatumbuliwa na  aliyepo ajipange, maana hakuna kinachoendelea wameshindwa kufufua viwanda.

“Kwanini hatuoni viwanda vikifufuliwa ,reli tunaona inafufuliwa, SGR tunaiona lakini huko kwenye viwanda hakuna chochote, kuna nini kwenye viwanda,” alihoji Dk. Bashiru

Katika hatua nyingine, Dk. Bashiru aliwataka viongozi dini, kuacha kutumiwa na wanasiasa kwa ajili ya kujipatia kiki kutoka kwa viongozi hao wa dini na badala yake waendelee kusimamia misingi ya haki na kulinda amani ya nchi.

Hayo aliyasema jana wakati akizungumza na viongozi wa dini, mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

“Ninazo taarifa wapo wanasiasa ambao wanatumia kiki kwa ninyi viongozi wa dini pamoja na waumini wenu, hivyo ninaowamba viongozi wa dini mtumike katika kuwaandaa kupata viongozi wazalendo na pia watakuwa wacha Mungu,” alisema Dk. Bashiru.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles