23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Benki ya Maendeleo Afrika kuipaisha daraja Tanzania

Na Waandishi wetu-Dodoma

BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), inatarajia kuipandisha daraja Tanzania kutoka  hadhi ya kunufaika na Mfuko wa Maendeleo wa Benki (ADF) hadi kuwa na hadhi itakayoiwezesha kupata rasilimali fedha zaidi kupitia dirisha la African Development Bank (ADB) la Benki ya Maendeleo ya Afrika.

Endapo Tanzania itafanikiwa kupandishwa hadhi, nchi itaweza kunufaika na ongezeko la fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika kutoka Dola za Marekani milioni 350 kwa mwaka hadi Dola milioni 812 kwa mwaka.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma jana na Mwakilishi Mkazi wa Benki hiyo, Dk. Alex Mubiru alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango .

Alisema hatua  ya kupandishwa hadhi ama kupandishwa daraja, inatokana na uchumi wa nchi kufanya vizuri hususani katika maeneo ya kasi ya ukuaji wa uchumi na kuwa na deni himilivu.

“Hatua hiyo itaiwezesha Tanzania kupata fedha zaidi kutoka katika Benki hiyo na kuwezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo na vipaumble kwa Serikali,” alisisitiza Mubiru.

Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Alex Mubiru, alisema benki hiyo inajivunia kufanya kazi na Tanzania ambayo ni miongoni mwa nchi waasisi wa benki hiyo.

Kwa upande wake, Dk. Mpango, alisema kuwa Serikali inajivunia kufanya kazi pamoja na Benki ya AfDB kwa kuwa benki hiyo imekuwa na masharti rafiki katika upatikanaji wa mikopo.

Alisema benki hiyo, ina mtazamo chanya katika maendeleo ya watu na kuwa dira katika mipango ya maendeleo na kuahidi kushirikiana nao vyema katika kukuza uchumi wa nchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles