23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

DAKTARI: TAULO YA KIKE INAWEZA KUSABABISHA UGONJWA WA MOYO

NA VERONICA ROMWALD  – DAR ES SALAAM

MATUMIZI ya muda mrefu ya taulo ya kike (pedi) wakati wa kipindi cha hedhi bila kubadilisha, yanaweza kumsababishia mwanamke kupata magonjwa mbalimbali ukiwamo wa moyo.

Hayo yalielezwa jana na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Jakaya Kikwete (JKCI), Bashir Nyangasa alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya moyo duniani  yanayofanyika  Septemba 29, kila mwaka.

“Kipindi cha hedhi ni muhimu mwanamke anatakiwa kuwa msafi ahakikishe anabadilisha ile pedi anayotumia kujihifadhi na si kukaa nayo kwa muda mrefu, ni hatari.

“Unapokaa na pedi kwa muda mrefu, ile damu ikajaa pale hutengeneza bakteria (wadudu), hapo una hatari ya kupata maambukizi kwenye kizazi, wale wadudu wanaweza kusafiri kwenda kuathiri moyo au figo zako,” alisema.

Alisema hatua hiyo kwa utaalamu inaitwa ‘entry point’ yaani hata ukijikata wadudu wanaweza kusafiri kwenda kwenye moyo wako na kuuathiri, hivyo ni muhimu kuzingatia usafi katika kipindi hicho.

Naye Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi hiyo, Tulizo Shemu aliwashauri wakazi wa   Dar es Salaam na maeneo jirani kujitokeza kwa wingi, katika taasisi hiyo kupima ugonjwa huo.

“Tutafanya upimaji bure na tutatoa elimu ya lishe, jinsi ya kujikinga na magonjwa ya moyo, kuanzia saa 2.00 hadi saa 10 jioni bila gharama yoyote,” alisema.

Alisema katika upimaji huo wananchi watapimwa urefu, uzito, shinikizo la damu (BP), sukari na  kupewa ushauri. Kwa wale watakaokutwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles