27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

CV KOCHA MPYA SIMBA TISHIO

  • Ni yule aliyeipa Cameroon ubingwa wa Afrika

Na MOHAMED KASSARA -DAR ES SALAAM

HATIMAYE klabu ya Simba imemtambulisha rasmi kocha wa zamani timu ya Taifa ya Cameroon Mfaransa, Pierre Lechantre, kuwa kocha mkuu wa kikosi hicho.

Lechantre ambaye aliiongoza Cameroon kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) mwaka 2000, anakuja kuchukua nafasi ya Joseph Omog, aliyetemwa baada ya timu hiyo kuvuliwa ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam.

Mfaransa huyo aliiongoza Cameroon kutwaa ubingwa huo baada ya kuichapa Nigeria kwa mikwaju ya penalti 4-3, katika mchezo wa fainali uliochezwa Februari 13 kwenye Uwanja wa Taifa Lagos, nchini Nigeria.

Mchezo huo ulifika hatua ya penalti baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 kwa kufungana mabao 2-2.

Katika mchezo huo, Cameroon iliwakilishwa na wachezaji mahiri kama Samuel Eto’o, Partick Mboma na Marc Vivian Foe ambaye kwa sasa ni marehemu, huku Nigeria ikiwa na Celestine Babayaro, Taribo West na Jay Jay Okocha.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 67, alichukua jukumu la kuinoa Cameroon kuanzia mwaka 1999 hadi 2001 alipotimkia Qatar.

Lechantre ambaye pia ni mshambuliaji wa zamani wa timu za FC Monaco na Olimpic Marseille za Ufaransa, amewahi  kutwaa tuzo mbili ya kocha bora Afrika  2001,  pia kocha bora Asia mwaka 2012.

Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara, ilisema kocha huyo ataanza kazi mara moja.

“Simba inayo furaha kubwa kuwajulisha wanachama na mashabiki wake kwamba, imempata kocha wake mkuu mpya, Mfaransa, Pierre Lechantre, kocha huyu ataanza kazi mara moja akisaidiwa na Masoud Djuma, aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo.

“Lechantre ameambatana na msaidizi wake, Mohammed Aymen Hbib, raia wa Morocco ambaye ni kocha wa viungo,” alisema Manara.

Wasifu kamili

KLABU ALIZOCHEZEA

1970-1975 Sochaux

1975-1976 Monac

1976-1979 Laval

1979-1980 Lens

1980-1981 Marseille

1981-1983 Reims

1983-1986 Red Star

1986-1989 Paris FC

TIMU ALIZOFUNDISHA

1987-1992 Paris FC

1992-1995 Le Perreux

1999-2001 Cameroon

2002-2003 Qatar

2003 Al-Ahli

2003-2004 Al-Siliya

2005-2006 Mali

2006-2007 Al Rayyan

2007-2008 MAS Fes

2009-2010 Club Africain

2010 CS Sfaxien

2012 AL Arabi

2014-2015 AL-Lttihad Club Tripoli

2016 Congo

 

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles