25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

“Corporate Unwind” ya Smartlab yalenga vijana kujifunza mbinu za kibiashara

MWANDISHI WETU

Kutokana na uhitaji viongozi shupavu wenye uelewa kuhusu teknolojia nchini, kampuni ya masuala ya kiteknolojia Smart Lab, imetoa wito kwa wamiliki wa makampuni na mashirika mbalimbali kuwekeza kwa vijana na wajasiriamali wabunifu ili kuisaidia serikali kupunguza tatizo la uhaba wa ajira nchini.

Wito huo umetolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Smart Codes, Edwin Bruno wakati akizungumza katika warsha iliyopewa jina la ‘Corporate Unwind’.

Warsha hiyo ambayo imefanyika kwa mara ya pili, hufanyika kila baada ya miezi mitatu kwa kuwakutanisha vijana wajasiriamali wabunifu wa masuala ya kitenlojia na wawekezaji au wamiliki wa makampuni waliofanikiwa ili kuwajenga kibiashara na kuwapatia mbinu za kukua zaidi kulingana na mawazo waliyobuni.

Bruno alisema Corporate unwind pia hulenga kujenga daraja kati ya wavumbuzi wakubwa na wachanga kwa kuwakutanisha pamoja na kujifunza mbinu mbalimbali za kukua kibiashara.

“SmartLab inafanya kazi hii kuhakikisha kuwa tunapata viongozi bora katika mifumo yetu ya uvumbuzi watakojenga kampuni zenye nguvu na mwishowe biashara imara, na hii ndiyo sababu tunatumia ujuzi na rasilimali zetu kwa kuwajenga uwezo wa vijana ili kupunguza tatizo la ajira.

“Hivyo ni muhimu makampuni na mashirika kutekeleza mikakati yenye kuwasaidia vijana wenye shida mbalimbali  kutoka kaya maskini hasa wasichana na kuelekeza nguvu katika utoaji elimu, ujuzi wa ajira na kujifunza ujasiriamali. Hili litaongeza mpango wa ushiriki sawa wa kijisni kimaendeleo na kukuza upatikanaji wa ajira,” alisema.

Alisema Corporate Unwind msimu huu imekuja na kauli mbiu inayosema “Uongozi bora unaochochea ukuaji kwenye sekta ya kibenki” inalenga kuwaandaa vijana kuwa viongozi bora katika sekta ya benki nchini.

Aidha, akizungumza katika jukwaa hilo, *Mzungumzaji mkuu wa misimu wa pili wa Corporate Unwind* ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Sanjay Rughani alisema, benki yake imelenga kutoa kipaumbele kwa vijana kujifunza maarifa mbalimbali katika sekta hiyo ili kukua kiuchumi.

“Tuna programu mbalimbali zinazowawezesha vijana kukua kibiashara, pia tunawafundisha namna kufanya kazi kutimiza ndoto zao.

“Nina furaha kuwa sehemu ya Corporate Unwind toleo la pili na pia ninafurahi kwa kupewa nafasi ya kujuana na hadhira ya watu ambao naamini wanapigania mabadiliko katika uchumi wa Tanzania na mfumo wa ubunifu kwa jumla” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles