25.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi wawaburuza Kortin watumishi 19

FARAJA MASINDE

Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB), imewakamata na kuwafikisha mahakamani watumishi 19 wa umma wakituhumiwa kwa kosa la kufanya kazi ya Ununuzi na Ugavi bila kusajiliwa na bodi hiyo jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Watumishi waliofikishwa mahakamani ni, Jema Mbogi, Julieth Daniel, Jeremiah Mafuru, Lucy Wanna, Odillo Benedict, Bihiana Romanus na Bahati Wonanndi.

Wengine ni, Raphael Waryana, Joseph Mhene, Victor Kilonzo, Moshi Mohammed,Avitus Rutuyug, Esther Rweymamu, Ruth Mwaipyana, Beatrice Mushi, Julieth Mwishambi, George Lyimo na Estonia Kalokola.

Akiwasomea shtaka hilo leo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Hudi Hudi, Mwanasheria wa Bodi(PSPTB), Suleiman Mnzava amedai mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na shtaka la kufanya kazi ya ununuzi na ugavi bila kusajiliwa na bodi ambalo walitenda kosa hilo kati ya Februari 11 na 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam kinyume cha sheria.

Watuhumiwa wote wamekana shtaka na kuachiwa kwa dhamana ya kuwa na wadhamini wawili waliosaini fungu la Sh. milioni tano mashrti ambayo wameyatimiza.

Kesi hiyo imeahirisha hadi Novemba 21, mwaka huu itakapo kuja kwa ajili ya kuanza kusikilizwa kwa hoja za awali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,526FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles