24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

CAVANI: NEYMAR NI SEHEMU YA FAMILIA

PARIS, UFARANSA

MSHAMBULIAJI wa klabu ya PSG, Edinson Cavani, amefunguka kwa mara ya kwanza juu ya mgogoro wake na mshambuliaji mwenzake, Neymar na kusema kwamba hakuna kibaya kinachoendelea kwa kuwa wapo hapo kama sehemu ya familia.

Wawili hao walikuwa kwenye mgogoro siku za hivi karibuni kutokana na kugombania nani mchezaji sahihi wa kupiga mipira ya adhabu nje kidogo na eneo la 18 pamoja na mipira ya penalti.

Cavani alikuwa mchezaji aliyepewa majukumu hayo yote kwa kipindi kirefu kabla ya ujio wa Neymar, lakini baada ya Neymar kusajiliwa kutokea Barcelona, akawa anataka awe yeye ndiye mpigaji kinyume na utaratibu jambo ambalo liliwaletea mgogoro mkubwa.

Juzi wawili hao waliisaidia timu yao kushinda mabao 3-0 dhidi ya Bayern Munich kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi, hivyo kila mmoja alifanikiwa kufunga bao na kuwafanya wachezaji waoneshe kuwa hawana tofauti yoyote inayoendelea kati yao, bao lingine liliwekwa wavuni na Dani Alves.

Baada ya kumalizika kwa mchezo huo juzi, Cavani aliongea kwa mara ya kwanza kwamba hana tofauti na Neymar kwa kuwa wote ni sehemu ya familia ya Paris Saint-Germain, lakini kila mmoja anafanya mambo yake binafsi nje ya uwanja.

“Ukweli ni kwamba mimi na Neymar hatuwezi kufanana kwa jambo lolote, tupo tofauti kabisa kuanzia kwenye maisha ya kila siku pamoja na mambo mengine, lakini tukiwa uwanjani lazima tuwe sawa kwa kuwa ni sehemu ya familia ya PSG.

“Hatuwezi kucheza soka kwenye klabu moja huku tuna mgogoro, kwa kufanya hivyo hatuwezi kuipeleka timu kokote, lengo letu ni kuhakikisha tunaipa PSG ubingwa na ndio maana kila mmoja amejitoa kwa hali na mali kuhakikisha timu inapata ushindi,” alisema Cavani.

Mbali na mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliowafanya Cavani na Neymar kuonesha kuwa wamemaliza tofauti zao, michezo mingine ambayo ilipigwa juzi ni pamoja na AS Roma iliyoshinda mabao 2-1 dhidi ya Qarabag FK, FC Basel ikishinda mabao 5-0 mbele ya Benfica, wakati huo Juventus ikishinda mabao 2-0 dhidi ya Olympiacos, Chelsea ikishinda mabao 2-1 dhidi ya Atletico Madrid.

Matokeo ya michezo mingine ni Man United ikishinda 4-1 dhidi ya CSKA Moscow, Celtic ikishinda mabao 3-0 dhidi ya Anderlecht pamoja na Barcelona ikishinda bao 1-0 dhidi ya Sporting.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles