23.6 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Bilioni mbili kusaidia mapambano dhidi ya Ukimwi

Amina Omari, Muheza

Serikali imetenga bajeti ya Sh bilioni mbili kwa ajili ya mapambano ya dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi ikiwemo uhamasishaji wa upimaji kwa hiari pamoja na matumizi ya dawa za kufubaza virusi vya ugonjwa huo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu na utaratibu wa ukimwi, Stella Ikupa wakati akiongea na waathirika wa ugonjwa huo Konga ya wilani Muheza.

Amesema kuwa bajeti hiyo imelenga katika kuhakikisha waathirika wanapata huduma bora za matibabu ikiwemo kinga na uwepo wa madawa ya kufubaza ukimwi.

“Serikali inahakikisha kila mwananchi hapa nchini ambaye anaishi na VVU kupata dawa, kuhamasisha umuhimu wa lishe sambamba na matumizi ya ARV “amesema.

Awali Katibu wa Baraza la Taifa la watu wanaoishi na Virus vya ukimwi Tanzania, Konga ya Muheza, Rose Kisaka amesema kuwa uwepo wa mradi wa sauti yetu umesaidia kuwarejesha kwenye utumiaji wa dawa za kufubaza kwa waathirika 212 walioko kwenye kata tano za mradi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles