25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Ngorongoro Heroes kamili kuimaliza Sudan

Winfrida Mtoi -Dar es salaam

TIMU ya Taifa ya vijana walio na umri chini ya miaka 20 ‘ Ngorongoro Heroes’, leo inashuka dimbani kuikabili Sudan, katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Chalenji ya Baraza la Vyama vya Soka kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), utakaochezwa mjini Gulu nchini Uganda.

Ngorongoro ilitinga hiyo, baada ya kuwatoa wenyeji Uganda kwa kuwachapa mabao 4-2, katika mchezo wa robo fainali uliopigwa  uwanja huo huo.

Ngorongoro ilizindua kampeni zake kwa kuifunga Ethiopia mabao 4-0, ikatoka sare ya 2-2 na Kenya kabla ya kuwamaliza ndugu zao Zanzibar ‘Karume Boys’, kwa kuwapiga mabao 5-0.

Hata hivyo mchezo dhidi ya Sudan hautakuwa rahisi kwa Ngorongoro, kwani wapinzani wao hao pia wameonyesha kiwango kizuri kwenye mashindano hayo.

Sudan ilikata tiketi hiyo baada ya kuwafunga majirani zao Sudan Kusini bao 1-0, katika mchezo wa robo fainali.

Ngorongoro inajivunia washambuliaji wake mahiri, Andrew Simchimba na Kelvin ambao wamejenga urafiki na nyavu.

Nyota hao kila mmoja amemefunga mabao sita kupitia michezo minne waliyocheza.

Pia kila mmoja amefanikiwa kuweka rekodi ya kufunga mabao  matatu ‘hat trick’ kwenye mmoja.

Akizungumzia mchezo huo, Kocha Mkuu wa Ngorongoro, Zuberi Katwila, alisema wamepata muda wa kutosha wa kupumzika hivyo anaamini wataikabili Sudan wakiwa na nguvu za kutosha.

Alisema hana wasiwasi na vijana wake, kwakua wamemuahidi kupambana katika hali yoyote ili kupata ushindi na kutinga fainali na hatimaye kutwaa ubingwa.

“Tunafahamu utakuwa ni mchezo mgumu wa nusu fainali, kila timu inahitaji kwenda mbele, Sudan ina kikosi kizuri nimekiona, lakini nimejipanga kama kocha na kuwapa maelekezo wachezaji wangu, kikubwa ni kucheza kwa nidhamu,” alisema Katwila.

Kwa upande wake John, alisema waliingia katika michuano hiyo wakiwa wamejiwekea malengo yao kama timu lakini pia binafsi.

Alisema kwa upande wake amejipanga kufunga  bila kujali idadi katika kila mchezo anaopata nafasi ya kucheza.

“Tumejipanga kama wachezaji kupambana, siri ya mafanikio yetu ni ushirikiano, ukipata nafasi ikiwa haupo nafasi nzuri ya kufunga unampa mwenzako, hasa mimi na Simchimba ambao mara nyingi tunacheza pamoja mbele.

“Mechi na Sudan ni ngumu lakini tutapambana na kujituma, tukifuata kile alichotuelekeza kocha wetu, naamini tutashinda,” alisema John.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles