24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Bil. 22 kujenga Chuo cha Veta Bukoba

Asha Bani, Dar es Salaam

Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, imesaini mkataba wa kuanza ujenzi wa chuo cha Ufundi Stadi (Veta), kinachotarajiwa kujengwa Bukoba mkoani Kagera kitakachogharimu Sh bilioni 22.4.

Fedha hizo zimetolewa na Serikali ya China katika kusaidia elimu ya ufundi nchini.

Akizungumza mara baada kutiliana saini ya kuanza ujenzi Katibu Mkuu wa Wizara hiyo  Dk. Leonard Akwilapo, amesema lengo ni kuhakikisha vijana wanapata elimu ya ufundi ili kuzalisha na kuongeza uchumi.

“Nchi inaelekea katika uchumi wa viwanda na serikali kupitia wizara yake itahakikisha inajenga vyuo vya ufundi nchi nzima kila mkoa. Chuo hiki cha Bukoba, kitakuwa kikubwa na kitakuwa na maeneo maalumu ya michezo, sehemu ya chakula na hata nyumba za walimu,” amesema Dk. Akwilapo.

Aidha, Dk. Akwilapo amewataka wanaosimamia ujenzi wa miradi ya elimu ikiwemo miundombinu, kuhakikisha inakwisha kwa wakati na kwamba hatosita kuwavunjia mkataba watakaoshindwa kufanya hivyo.

Naye mwakilishi kutoka nchini China nchini anayesimamia masuala ya uchumi na biashara, Lin Yuan, amesema wameamua kufanya hivyo kutokana na ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na China huku akiahidi kuendelea kusaidia katika nyanja mbalimbali za kijamii.

Mkurugenzi Mkuu wa Veta, Pancras Bujulu amesema lengo ni kutaka vyuo hivyo viwe nchi nzima ili kuwafanya vijana kuajiriwa na kuwa na uwezo wa kujiajiri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles