Imechapishwa: Sat, Jun 9th, 2018

BEYONCE, JAY-Z WAFUNGA NDOA TENA

 

CARDIFF, WALES

MASTAA wa muziki nchini Marekani, Beyonce na mume wake Jay Z, wametikisa mitandao ya kijamii wiki hii baada ya kuionesha ndoa yao kwenye jukwaa la ‘On The Run II Tour’ mjini Cardiff na kudai wanafunga upya.

Wanandoa hao wapo kwenye ziara yao ya muziki barani Ulaya na Jumatano wiki hii walikuwa Cardiff kwa ajili ya shoo yao, hivyo walitumia nafasi hiyo kuwaonesha mashabiki wao jinsi walivyofunga ndoa Aprili 4, 2008.

Walitumia runinga kwenye shoo hiyo kwa ajili ya kuwaonesha mashabiki wao jinsi harusi hiyo ilivyokuwa ya siri.

“Naamini watu wengi hawakuona jinsi tulivyofunga ndoa mwaka 2008, hii ni nafasi pekee ya kuiona kwa kutumia runinga zetu humu ndani, kwa kufanya hivi ni sawa tunafunga ndoa tena,” alisema Jay Z.

Ziara hiyo imeanza wiki hii na inatarajiwa kufikia mwisho Oktoba, mwaka huu huku wawili hao wakitarajia kufanya jumla ya shoo 48.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

BEYONCE, JAY-Z WAFUNGA NDOA TENA