23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS NKURUNZIZA AZUA GUMZO BUJUMBURA, BURUNDI

UAMUZI wa Rais Pierre Nkurunziza kutowania muhula mwingine katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2020, umeibua mijadala mikubwa ndani na nje ya Burundi.

Kauli ya Nkurunziza inakuja baada ya kuonyesha nia mapema ya kuendelea madarakani hasa katika kile alichokuwa akieeleza katika hotuba zake za nyuma kwamba alichaguliwa na Mungu kuhudumu.

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa Rais huyo ameeleza hatowania muhula mwingine katika uchaguzi wa mwaka 2020 ikiwa na maana chama chake kinatakiwa kuandaa mrithi wa nafasi hiyo.

Muungano wa vyama vya CNARED unasema mzozo wa Burundi si Nkurunziza, bali ni katiba ya Arusha ambayo imebadilishwa na kwamba anachokifanya Nkurunziza ni kuuzubaisha umma, kama anavyoeleza hapa Pancras Cimbaye msemaji wa Cenared.

Lakini swali tete ambalo limeendelea kuibuka ni kwanini Rais Nkurunziza amebadili msimamo wake na je, ataheshimu kauli yake?

Wataalamu wanaona kuwa huenda ni kukosa uungwaji mkono wa viongozi wa ukanda, pamoja na mzozo wa ndani ya chama chake cha CNDD-FDD zikiwa ni miongoni mwa sababu za kubadili msimamo wake.

Hata hivyo, wachambuzi wa masuala ya siasa wanaona kuwa kauli ya Nkurunziza inadhihirisha wazi kwamba hali ni tete upande wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles