Beyonce anyakua tuzo saba za MTV-VMA

0
219

BeyonceNEW YORK, MAREKANI

NYOTA wa muziki nchini Marekani, Beyonce Knowles, amefunika kwenye tuzo za MTV Video Music Awards 2016, kwa kuondoka na tuzo saba.

Nyota huyo wa muziki ambaye ni mke wa rapa Jay Z, alikuwa na furaha kubwa kwa kuweka historia kwa mwaka huu katika usiku wa kuamkia jana zilipofanyika tuzo hizo.

“Nianze kwa kumshukuru mtoto wangu na mume wangu Jay Z kwa sapoti yao, hata hivyo nawashukuru wote mlio pamoja nami katika kazi za muziki wangu, leo ni siku ya furaha kubwa kwangu kwa kupata tuzo nyingi, nawashukuru sana,” alieleza furaha yake Beyonce.

Mrembo huyo aliingia kwenye vinyang’anyiro nane lakini alifanikiwa kuondoka na tuzo saba.

Tuzo alizozichukua ni pamoja na Video bora ya mwaka ‘Formation’, video bora kwa wasanii wa kike ‘Hold Up’, video bora ya Pop ‘Formation’, video iliyoweka historia kwa muda mrefu ‘Lemonade’ Sinema bora ‘Formation’ na Uhariri bora ‘Formation

Msanii huyo amewafunika nyota wengi akiwemo Drake, Rihanna, Justin Bieber, Adele na wengine.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here