Imechapishwa: Fri, Jan 12th, 2018

AZAM FC: KOMBE HALIONDOKI TANZANIA

NA MWANDISHI WETU-ZANZIBAR

KOCHA Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba, amesema hawatarudia tena makosa zaidi ya kuhakikisha wanaifunga URA na kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi.

Azam imefuzu hatua ya fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya juzi kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Singida United, mchezo uliochezwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Akizungumza na MTANZANIA, Cioaba alisema baada ya kupoteza dhidi ya URA katika hatua ya makundi, wapinzani wao hao wasitarajie kupata mteremko katika fainali, kwani tayari wamejua kilichowagharimu awali.

Alisema baada ya kuibwaga Singida atahakikisha anarekebisha kasoro zilizojitokeza kabla ya kuikabili URA.

“Tunahitaji kushinda mechi hiyo ili kutetea ubingwa wetu, tunaenda kujiandaa kwa ajili ya fainali hiyo,” alisema kocha huyo.

Wakati huo huo mfungaji pekee wa bao la Azam, Shaban Iddi, amesema atahakikisha anatumia vema nafasi atakayopata kufanya kazi vizuri itakayomfanya azidi kuaminiwa na kocha wake huyo.

“Nimetoka katika majeruhi makubwa, kocha analazimika kunipa dakika 10 hadi 25 ili taratibu nirudi katika hali yangu, nitahakikisha natumia vema kila nafasi ninayopata ili kuonyesha heshima kwa kocha wangu na kuwafurahisha mashabiki wetu,” alisema Shaban.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

FACEBOOK

YOUTUBE

Translate »

AZAM FC: KOMBE HALIONDOKI TANZANIA