24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

MATOLA ATIMKA LIPULI FC

NA MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

KOCHA wa msaidizi wa Lipuli FC, Seleman Matola,ameikacha timu hiyo na kurejea Dar es Salaam baada ya kutokea tofauti ya kimtazamo na  kocha mkuu wa timu hiyo, Amri Said.

Kutoelewana kati ya makocha hao ambao pia waliwahi kuitumikia Simba kama wachezaji kulitokea katika kikao kilichofanyika juzi kwaajili ya maandalizi ya michezo ijayo ya Ligi Kuu Tanzania Bara ya timu hiyo.

Akizungumza na MTANZANIA,Said alithibitisha kutokea kwa jambo hilo,lakini akasema halikuwa jambo kubwa kiasi cha kocha mwenzake kufikia hatua hiyo.

“Juzi katika kikao chetu kulitokea kutoelewana na mwenzangu, tulipishana kauli kwa ajili ya vitu vidogo sana, ambavyo sikudhani kama vingeleta tatizo.

“Leo (jana) katibu alinionyesha ujumbe ambao ulitumwa na Matola ukieleza ameamua kuondoka kurudi Dar es Salaam, kitu ambacho kimenishangaza sana, tulikuwa tunajadili maandalizi ya mechi zetu za ligi, lakini ikatokea kitu kidogo tu ndio kimeleta shida” alisema Amri Said.

Katibu Mkuu wa Lipuli FC Willy Chikweo, alisema kilichotokea ni jambo la kawaida  katika mazingira ya kazi.

“Nijambo dogo sana ambalo siwezi hata kulizungumzia sana kwa kuwa wale ni ndugu wamecheza pamoja Simba wamekaa chumba kimoja, yaani ni zaidi ya marafiki,naamini yataisha,” alisema Chikwao.

Alisena anaimani Matola ataendelea kufanya nao kazi licha ya kutokea hali hiyo ya kutoelewana kati yake na Saidi.

Lipuli inashika nafasi ya nane katika msimamo wa Ligi kuu Tanzania  Bara ikiwa imejikusajia pointi 14 kupitia michezo yake 12 iliyocheza mpaka sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles