25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Aveva kukabidhiwa ofisi Julai 8

Evans Aveva
Evans Aveva

NA KAMBI MBWANA, DAR ES SALAAM

UONGOZI wa zamani wa klabu ya Simba unatarajia kumkabidhi ofisi rais mpya wa klabu hiyo, Evans Aveva, Julai 8 sambamba na kuanika mambo yote, ikiwamo Sh milioni 420 zilizotajwa na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Ismail Aden Rage.

Siku ya Uchaguzi Mkuu, Rage alitangaza kwa waandishi wa habari kuwa anaondoka madarakani akiwa amemuachia rais mpya Sh Milioni 420, jambo ambalo limepokewa kwa hisia tofauti na wadau na mashabiki wa soka.

Habari zilizopatikana jana jijini zinadai Rais huyo ameacha mali kauli na hakuna pesa kwenye akaunti benki, bali ametaja pesa ambazo hazipo mkononi za malipo ya pango klabuni hapo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Simba anayemaliza muda wake, Ezekiel Kamwaga, alisema kwa sasa taratibu za ofisi hiyo zinaandaliwa kwa ajili ya kumkabidhi Rais huyo ofisi kwa ajili ya kuongoza baada ya kuchaguliwa kwa kishindo na wanachama wake.

Alisema anaamini pamoja na Sh Milioni 420 zilizotajwa na Mwenyekiti Rage, Simba pia ina mambo mengi ambayo kisheria lazima yaandaliwe kwa ajili ya kumpa mwanga wa utendaji wake kwa maendeleo ya klabu yao.

“Makabidhiano rasmi ya ofisi yamepangwa kufanyika Julai 8, ambapo taratibu zote zitawekwa hadharani kuhusu hizo Milioni 420, ni vyema pia wadau wakasubiria siku hiyo ya makabidhiano kwasababu kila kitu kitawekwa hadharani, ili kuhakikisha kuwa mambo yanakwenda sawa na kuiletea maendeleo klabu,” alisema Kamwaga.

Aveva ndiye rais wa kwanza wa klabu hiyo tangu Katiba ya Simba iliposajiliwa na kuondoa neno mwenyekiti na kutambulika kama Rais, akirithi mikoba ya Rage, huku wanachama wengi wakiwa na imani naye.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles