ALISSON AWAOMBA RADHI LIVERPOOL

0
695LIVERPOOL, ENGLAND

MLINDA mlango wa klabu ya Liverpool, Alisson Becker, ameiomba radhi klabu hiyo kutokana na makosa aliyoyafanya juzi kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Leicester City.

Katika mchezo huo, Liverpool ilifanikiwa kuongoza mabao mawili hadi kipindi cha pili, lakini kipa huyo ambaye amesajili kwa kiasi kikubwa cha fedha katika kipindi hiki cha majira ya joto, alifanya uzembe kwa kujaribu kumpiga chenga mshambuliaji wa Leicester City, Kelechi Iheanacho na hatimaye kujikuta akipokonywa mpira na kufungwa bao.

Hivyo mchezo huo ulimalizika kwa Liverpool kushinda mabao 2-1, lakini kipa huyo alijutia kosa hilo na kuomba radhi mashabiki na Liverpool kwa ujumla huku akidai kwamba amejifunza kutokana na makosa na hawezi kurudia tena kosa hilo.

Tukio kama hilo kwa Liverpool lilitokea kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid, ambapo kipa wa klabu hiyo Loris Karius, alifanya kosa kama hilo na kusababisha timu hiyo kufungwa.

“Nimefanya kosa kubwa sana ambalo kila mmoja analielezea kwa namna yake, hivyo naweza kusema siwezi kufanya tena kosa kama hilo, tunatakiwa kujifunza kutokana na makosa, lakini hiyo ilikuwa ni sehemu ya mchezo.

“Nilijisikia vibaya sana kwa kuwa timu niliiweka katika wakati mgumu, lakini ninashukuru tuliweza kupambana na kulinda ushindi wetu,” alisema Alisson.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here