RONALDINHO AMTAKA NEYMAR BARCELONA

0
1088BARCELONA, HISPANIA

NGULI wa soka wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya Barcelona, Ronaldinho Gaucho, ameweka wazi kwamba, atakuwa na furaha sana endapo staa wa taifa hilo Neymar, atarudi katika klabu yake hiyo ya zamani.

Neymar alikuwa katika klabu ya Barcelona kwa kipindi cha miaka minne kabla ya mwaka jana kujiunga na klabu ya PSG ya nchini Ufaransa kwa uhamisho wa kitita cha pauni milioni 198, alidaiwa kuondoka Barcelona kutokana na kushindwa kutamba mbele ya Lionel Messi.

Hata hivyo Neymar amekuwa na mchango mkubwa ndani ya PSG tangu alipojiunga japokuwa alikuwa majeruhi, lakini kumekuwa na taarifa kwamba mchezaji huyo anataka kurudi kucheza soka la nchini Hispania hasa klabu ya Real Madrid.

Kutokana na taarifa hizo, Ronaldinho amedai kwamba, atakuwa na furaha sana endapo atamuona nyota huyo akirudi katika klabu yake ya zamani ya Barcelona kuliko Real Madrid.

“Kitu muhimu kwa Neymar ni furaha. Napenda kumuona rafiki yangu akiwa na furaha, lakini kwa upande wangu nitakuwa na furaha zaidi endapo nitamuona mchezaji huyo akirudi Barcelona. Hata hivyo sina uhakika kama jambo hilo linaweza kutokea,” alisema Ronaldinho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here