23.6 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Airtel yazindua simu mpya ya iPhone 5s

Simu aina ya iPhone S5
Simu aina ya iPhone S5

KAMPUNI ya simu ya Airtel imetangaza ushirika wake na kampuni kubwa inayotengeneza simu za mkononi ya Apple. Kutokana na ushirikiano huo, Airtel imeweka historia kwa kuwa kampuni ya kwanza ya mawasiiliano Tanzania kuingia mkataba na Apple kupitia simu ya iPhone S5.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana baada ya uzinduzi huo wa simu, Meneja Masoko wa Airtel, Prisca Tembo alisema uzinduzi huo umelenga kuwapatia wateja wao bidhaa.

“Leo (jana) tunazindua simu ya iPhone 5s na kuwapatia wateja wetu ofa kabambe ya vifurushi vya muda wa maongezi, ujumbe mfupi na internet. Mteja atakaponunua simu ya iphone S5 atapata kifurushi cha internet cha 3GB, dakika 1450 za maongezi na SMS 5000 kwa mwezi.

“Natoa wito kwa Watanzania na wateja wetu kutembelea maduka yetu na mawakala wetu ili kuweza kujipatia simu hii,” alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Beatrice Singano alisema: “Uzinduzi huu utatoa fursa kwa wateja wetu kupata uzoefu tofauti wa huduma zetu na kuwawezesha kuendelea kufurahia huduma yetu ya SWITCH on,” alisema.

“Simu hii ya iPhone 5s itawawezesha wateja wetu pia kupiga picha, kutuma video na kuwaunganisha na marafiki na familia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles